Home » » MAAMBUKIZI VVU YAPUNGUA

MAAMBUKIZI VVU YAPUNGUA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

MAAMBUKIZI ya virusi vya Ukimwi (VVU), kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto yamepungua kwa asilimia 90. Imeelezwa.
Hayo yalisemwa na Meneja wa shirika la EGPAF Mkoa wa Tabora, Dk. Alphaxard Lwitakubi, mara baada ya Rais Jakaya Kikwete kukagua banda la shirika hilo katika maonyesho ya wiki ya vijana iliyoambatana na kilele cha kuzimwa kwa Mwenge wa Uhuru.
Lwitakubi, alisema lengo la EGPAF ni kufikia asilimia 98 ifikapo mwishoni mwa mwaka 2015.
Alisema hatua hiyo itafikiwa endapo wanaume wataambatana na wake zao kwenda kwenye vituo vya afya kama inavyotakiwa, kwani hadi sasa zimefikiwa asilimia 48 kwa mwaka 2014 kutoka asilimia 5 mwaka 2010.
Dk. Lwitakubi, alisema Shirika la EGPAF limekuwa likijihusisha na kazi za kuzuia na kutokomeza maambukizi ya virusi vya Ukimwi (VVU), kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.
Alisema EGPAF inafanya kazi zake katika mikoa ya Tabora, KilimanjaroArusha, Lindi, Shinyanga, Geita na Simiyu.
Aliongeza kuwa EGPAF pia imekuwa ikijihusisha na wagonjwa wa majumbani katika mikoa ya Pwani, Zanzibar na Mwanza huku likitoa huduma za uchunguzi wa
saratani ya shingo ya kizazi mikoa ya Tabora, Kilimanjaro,
Shinyanga, Arusha, Simiyu, Lindi na Geita.

Kwa upande wake, Mratibu wa Mawasiliano na Utetezi wa EGPAF, Mercy Nyanda, alisema katika huduma zao kumekuwa na mafanikio, kwani kwa sasa wajawazito wengi wanajifungulia vituoni tofauti hapo mwanzo.
Nyanda, alisema uelewa kwa jamii umeongezeka zaidi kuhusu hali halisi ya maamukizi ya VVU na jamii hiyo kuendelea kubadilika.
Chanzo;Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited : |
Copyright © 2012. Tabora Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za mikoa