Home » » JESHI LA ANGA LA CCM LAMALIZA KAZI TABORA,WANANCHI WAAHIDI KUCHAGUA "KAZI TU"

JESHI LA ANGA LA CCM LAMALIZA KAZI TABORA,WANANCHI WAAHIDI KUCHAGUA "KAZI TU"

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Mwigulu Nchemba akisalimiana na Wananchi katika moja ya Majimbo mkoa wa Tabora hii leo wakati wa ziara yake ya kuzunguka Mkoa wa Tabora wote kwaajili ya kuinadi Ilani ya Chama cha Mapinduzi na Kuwaombea Kura Madiwani,Wabunge na Rais mtarajiwa wa Chama cha Mapinduzi.Mwigulu Nchemba katika harakazi za kuhakikisha CCM inashinda kwa kishindo kwa Mkoa wa Tabora na Nchi nzima hii leo akiwa Tabora Jimbo la Igunga.Chagua Almasi Maige kwa Maendeleo ya Tabora Kaskazini.Mjumbe wa timu ya Ushindi ya CCM Taifa Comrade Mwigulu Nchemba akimnadi Mgombea wa Jimbo la Igagula Ndg.Ntimizi hii leo alipofika kwaajili ya kuinadi Ilani ya CCM na kuwasihi Watanzania walipojo Tabora kuichagua CCM kwenye Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Mwishoni mwa October 2015.Chagua Ntimizi kwa Jimbo la Igagula -Tabora.Mbunge Mtarajiwa wa Urambo Bi.Magret Sitta akiomba kura kwa Wananchi wake wa Urambo.Dr.Hamis Kigwangalla akisalimiana na Wananchi wa Urambo kata ya pembezoni na Mji wa Urambo.Kigwangalla amewasihi wananchi wa Urambo kuachana na Wagombea waigizaji ilihali wameitumikia Serikali ya CCM kwa muda mrefu na kulisababishia Taifa hasara kubwa,Leo wamekimbia CCM na kujivika ngozi ya kondooo wakiwa upinzani.Hivyo wananchi wote wawapuuze na wamchague Magufuli na Wabunge wa CCM kwaajili ya Serikali mpya yenye Fikra mpya.Mwananchi wa Urambo akionesha kipeperushi cha Kumuunga Mkono Mgombea Ubunge wa Jimbo hilo Bi.Magret Sitta.Mwigulu Nchemba akiondoka Jimbo la Urambo FieldMashall Mwigulu Nchemba akizungumza na Wananchi wa Sikonge hii leo Mkoani Tabora wakati wa Mkutano wa Kampeni wa Chama Cha Mapinduzi,Mwigulu Nchemba amewasisitiza Wananchi wa Sikonge Kuachana na siasa za Makundi ndani ya Chama Cha Mapinduzi,"Wananchi wote,WanaCCM wote tuunganishe nguvu zetu kukipa Ushindi chama cha Mapinduzi,Tuunganishe nguvu kuhakikisha tunapata Mbunge wa CCM atakayeweza kutatua Matatizo ya Tumbaku hapa Sikonge"
Mbali na hilo ,Mwigulu Nchemba ameendelea kusisitiza Uchaguzi wa Amani na Upendo kwa vyama vyote,Amewasihi Wananchi wajitokeze kupiga Kura ilikuwachagua Madiwani,Mbunge na Rais wa Chama cha Mapinduzi wenye Ilani inayotekelezeka.Mwigulu Nchemba akimnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Sikonge kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi.Said Nkumba aliyekuwa Mbunge wa sikonge akimnadi Mgombea Ubunge wa CCM Jimbo la sikonge kuuonesha wazi Umma kuwa CCM kwa Sikonge ni Moja.Vijana wa kazi wa Chama Chama Mapinduzi Ndg.Mwigulu Nchemba na Hamis Kigwangalla wakionesha Umahili wao wa kupiga Push-Up kabla ya Kuanza kwa Mkutano wa hadhara Jimbo la Sikonge hii leo Mkoani Tabora.CCM na Vijana wake wa kazi wakiwa na kofia za Kijamaa.Mwigulu Nchemba akiagana na Wananchi wa Jimbo la Sikonge waliofurika kusikiliza sera za Chama cha Mapinduzi kuelekea Uchaguzi Mkuu 2015.
Picha na Sanga Festo Jr

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited : |
Copyright © 2012. Tabora Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za mikoa