Home » » Dr.Amon Mkoga Foundation wakabidhi madawati 90 kwa wilaya ya Tabora mjini.

Dr.Amon Mkoga Foundation wakabidhi madawati 90 kwa wilaya ya Tabora mjini.



Afisa Tawala Wilaya ya Tabora mjini Mhe. Sweetbert Nkuba, (kushoto) akipokea moja ya madawati 90 yaliyotolewa na Dr.Amon Mkoga Foundation  na kukabidhiwa kwake na mwenyekiti wa Taasisi hiyo Ndugu.Amon Mkoga(kulia). Anayeshuhudia  ni Mkuu wa Kitengo cha uhusiano na Uhamasishaji wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bi. Sarah Kibonde Msika ambao ni wadhamini wa kampeni hiyo iitwayo “Simama Kaa”

 Ndugu.Amon Mkoga akiwa pamoja na wanafunzi hao baada ya kukabidhi madawati hayo
 Ndugu.Amon Mkoga akiwa amekaa na baadhi ya wanafunzi baada ya kukabidhi madawati hayo
Taasisi ya Dr.Amon Mkoga Foundation imetoa msaada wa madawati 90 yenye thamani ya shilingi milioni 5.5 kwa shule za msingi katika manispaa ya Tabora, ikiwa ni mchango wa Taasisi  hiyo katika kuisaidia serikali kukabiliana na upungufu wa madawati katika shule za msingi nchini. 
Akizungumza leo katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika ofisi ya mkuu wa wilaya Tabora mjini , Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Ndugu Amon Mkoga amesema mchango huo ni sehemu ya utekelezaji wa dhamira ya taasisi  hiyo ya kuunga mkono jitihada mbalimbali za kuleta maendeleo nchini.
“Mchango huu ni sehemu ya jitihada mbalimbali zinazofanywa na Dr.Amon Mkoga Foundation  katika kusaidia utekelezaji wa miradi yenye tija kubwa kwa jamii. Tunaamini kwamba kupitia msaada huu, Taasisi yetu inatoa mchango wake katika kujenga viongozi wa baadaye wa taifa hili na wanataluuma mbalimbali wakiwamo madaktari, wahandisi na wengineo, “amesema Mkoga.
 
Makabidhiano yalihudhuriwa na Afisa Tawala Wilaya ya Tabora mjini Mhe. Sweetbert Nkuba ambaye alisema madawati hayo 90 yataboresha mazingira ya kujifunzia kwa watoto katika Mkoa wa Tabora na kutoa wito kwa wadau wengine kuunga mkono zoezi hilo.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited : |
Copyright © 2012. Tabora Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za mikoa