Home » » DKT. TIZEBA LIMENI MIHOGO SOKO LIPO NA TIGANYA VINCENT RS-TABORA

DKT. TIZEBA LIMENI MIHOGO SOKO LIPO NA TIGANYA VINCENT RS-TABORA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


WAKAZI Mkoani Tabora wametakiwa kulima mazao ya korosho na mihogo kwa ajili kujiongezea kipato ambacho kitawawezesha kuboresha maisha yao na kujiinua kiuchumi.
Kauli hiyo imetolewa jana wilyani Uyui na Waziri wa Kilimo Dkt. Charles Tizeba wakati alikwenda kuangalia maandalizi ya kilimo cha zao hilo na kampeni za uhamasishaji wananchi kulima kwa wingi zao hilo zinazoendeshwa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora.
Alisema kuwa mazao hayo pia yatawasaidia wakulima kujikwamua kiuchumi kwa sababu yanahitajika sehemu mbalimbali duniani.
Dkt. Tizeba alisema kuwa hivi sasa zao la korosho linabei nzuri na ndilo limeongoza kwa kuingiza fedha za kigeni hapa nchini.
Alisema kuwa wakulima wote wanaohitaji kulima zao hilo ni vema wakajiandikisha kwa Maofisa Kilimo wa Wilaya kwa ajili ya kupata michezo ya zao hilo.
Waziri huyo aliongeza kuwa katika hekta miche inayohitajika ni 27 hadi 33 na inaanza kuvunwa baada ya miaka mitatu na wakulima wataendelea kufaidika kwa kipindi cha miaka 50 ijayo baada ya upandaji.
Alisema kuwa hivi sasa wakati wa maeneo ya Pwani maisha yao yamekuwa mazuri kwa sababu ya zao hilo na kuongeza kuwa ni fursa kwa wakazi wa Tabora kuanza kulima zao hilo.
Dkt. Tizeba aliwaeleza wakazi wa Tabora kuwa tayari Serikali imeshaleta mbegu za korosho mkoani humo kwa ajili ya wakulima ambao wako tayari kulima zao hilo kuanza kupanda.
Kuhusu zao la Mhogo alisema kuwa hivi sasa linahitajika sehemu mbalimbali duniani la kulifanya kuwa zao la biashara.
Alisema kuwa udongo wa Tabora unastawi mihogo ni vema wakatumia fursa hiyo kulima kwa wingi na hasa mbegu inakabiliana na ugonjwa mbalimbali.
Alisema kuwa nchi mbalimbali zimekuwa zikiitaji mihogo na hivyo kutoa fursa kwa zao hilo kuwa la biashara.
Dkt. Tizeba aliwaagiza Maofisa Ugani kuwasaidia wakulima kupata mbegu za mihogo ambazo zinazokabiliana na ugonjwa kutoka katika Chuo cha Kilimo Tumbi na maeneo mengine ili wakulima waweze kuchamkia fursa hiyo kwa ajili ya kuboresha maisha yao na kuleta fedha za kigeni.
Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri alisema kuwa mkoa huo umeamua kulima kwa wingi mazao kama vile korosho, pamba, tumbaku , alizeti na mazao mengine yakiwemo ya chakula kwa ajili ya kupata malighafi za kutosha kwa ajili ya viwanda vilivyopo na vitakavyoanzishwa.
Alisema kuwa kwa upande wa alizeti kila familia itapaswa kulima ekari mbili kwa ajili ya kuwa na mazao ya kutosha ambayo yatawavutia wawekezashaji katika Kiwanda cha kusindika mafuta ya alizeti.
Mwisho

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited : |
Copyright © 2012. Tabora Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za mikoa