Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
a
Jeshi la Polisi Kikosi cha FFU
Mkuu wa zamani wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU)
mkoani Tabora, Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP), Bhoke Bruno na polisi
wawili, wamefikishwa mahakamani kujibu shitaka la upotevu wa bunduki
nane aina ya Sub Machine Gun (SMG) mali ya Jeshi la Polisi.
Walifikishwa jana katika Mahakama ya Mkoa wa Tabora.
Washtakiwa wengine waliofikishwa mbele ya Hakimu Mfawidhi wa
mahakama hiyo, Issa Magoli, ni Koplo Iddi Abdallah na Mwinyi Gonga, wa
Kikosi cha FFU Tabora.
Akiwasomea mashitaka, Wakili wa Serikali, Juma Masanja, alidai kuwa
washtakiwa wote watatu wanakabiliwa na shitaka moja la kutochukua
tahadhari stahiki katika utunzaji wa silaha.
Alidai kuwa watuhumiwa hao walitenda kosa hilo kati ya Aprili,
mwaka jana na Aprili, mwaka huu wakiwa waajiriwa wa Jeshi la Polisi
Kikosi cha FFU Tabora.
Wakili Masanja alidai kuwa washtakiwa kwa pamoja walishindwa
kutumia njia za kiusalama katika utunzaji wa silaha na matokeo yake
bunduki nane aina ya SMG ziliangukia katika mikono ya watu ambao si
wamiliki halali wa silaha hizo.
Watuhumiwa wote walikana shitaka na kurejeshwa mahabusu baada ya
kunyimwa dhamana kutokana na Wakili wa Serikali kupinga dhamana kwa hofu
ya kuingilia upelelezi pale watakapokuwapo nje.
CHANZO:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment