NA TIGANYA VINCENT
RS TABORA
26 February 2018
WAZIRI
Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mkuu wa Chuo Kikuu
Huria cha Tanzania(CKHT) Mizengo Pinda ametoa wito kwa Wataalamu wa Chuo
hicho kutoa mafunzo ambayo yatawasaidia wananchi kuleta mageuzi ambayo yatawezesha katika ujenzi wa Tanzania ya Viwanda na hivyo kutimiza lengo la Serikali ya Awamu ya Tano.
Mkuu huyo wa Chuo Kikuu hicho alitoa kauli hiyo mjini hapa wakati akizungumza na Watumishi na Wanachuo wa CKHT Tawi la Tabora wakati wa ziara ya siku moja chuoni hapo.
Alisema
kuwa Chuo hicho kinayo nafasi kubwa ya kuleta mageuzi yatakawawezesha
wananchi wengi waweze kutoa mchango wao katika ujenzi wa uchumi wa
viwanda hapa nchini na hivyo kusaidia katika mapambana dhidi ya
umaskini.
Mkuu
huyo wa Chuo hicho alisema kuwa hiyo itawezekana ikiwa elimu
itakayotolewa itakuwa ikisaidia katika kujibu matatizo ya wananchi kwa
kuwa na wahitimu ambao wanaweze kuwa mfano kwa wananchi ili waweze
kujifunza kwao mbinu zitakazowawezesha kujiletea maendeleo.
Aidha
Waziri Mkuu huyo Mstaafu aliwataka Watendaji na wadau mbalimbali
kusaidia kuwahamasisha walimu wengi hasa wa shule za Msingi kujiunga na
Chuo hicho katika maeneo mbalimbali ili waweze kujiendeleza zaidi na
kuboresha mbinu za ufundishaji.
Alisema
kuwa Chuo Kikuu Huria kikitumiwa vizuri kinamchango mkubwa wa kuleta
mageuzi katika sekta ya elimu na nyingine na kuweza kuboresha ufaulu
hata katika maeneo ambayo wanafunzi walikuwa hawafanyi vizuri katika
mitihani yao ya kumaliza elimu ya msingi.
Waziri
Mkuu huyo Mstaafu aliongeza kuwa hatua itasaidia sana kuleta tija
katika mbinu ufundishaji itakayoasaidia katika kuongeza ufaulu wa
wanafunzi wote hata wale wenye mahitaji maalumu.
Katika
hatua nyingine Mkuu huyo wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania amewaagiza
Wataalamu wake kuangalia jinsi ya kuandaa utaratibu na vigezo vya
upimaji wa vituo mbalimbali katika matawi yake nchini ili kuona ni Kituo
gani kimefanya vizuri na Kituo cha mwisho.
Alisema
kuwa hatua hiyo itawasaidia kujua kama Kituo kimekuwa cha mwisho sababu
ni nini na kama ni walimu waweze kutatua na hivyo kufanya waweze nao
kufanya vizuri.
“Kama
tunavyofanya katika elimu ya msingi na sekondari , nimeagiza Wataalamu
waangalie jinsi ya kuanza kupima ufaulu wanachuo wetu katika Vituo vya
Chuo Kikuu Huria ili tujue cha kwanza na cha mwisho…kama kituo kitakuwa
cha mwisho tujue na sababu, kama ni udhaifu wa wakufunzi tuweze
kulifanyia kazi” alisema Mkuu huyo wa Chuo.
Naye
Mkurugenzi wa CKHT Tabora Noel Nkombe alisema kuwa Tawi hilo
linakabiliwa na tatizo na ukosefu wa majengo kwa ajili ya utoaji wa
huduma kwa wanachuo , jambo ambalo limewafanya wafanye kazi kwa kuhama
hama mara kwa mara.
Alisema
kuwa ili kukabiliana na tatizo hilo tayari wamepata kiwanja katika eneo
la Ipuli katika Manispaa ya Tabora ambapo katikati ya mwezi ujao
wanatarajia kuendesha harambee kwa ajili ya kupata fedha za kuanza
ujenzi wa awali.
Akisoma
risala ya wanachuo Katibu wa Serikali ya Wanachuo Tawi la Tabora Husna
Suleyman alisema kuwa kwa kutambua tatizo la majengo kwa ajili ya Kituo
chao , wao kwa hiari hayo wameamua kuchanga kila mmoja shilingi 30,000
ambapo zimepatikana milioni 6.1.
Alisema kuwa hatua hii inalenga kuunga mkono juhudi za uongozi wa CKHT za kutaka kuboresha mazingira ya wao kujisomea.
mwisho
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment