Wanakikundi cha Upendo kilichopo
Kijiji cha Magiri Kata ya Magiri katika Halmshauri ya Wilaya ya Uyui
mkoani Tabora wakiwa pamoja na watafiti kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi
na Teknolojia (COSTECH), Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo
(OFAB), Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha ARI-Maruku mkoani Kagera na
Mwanahabari Coleta Makulwa wa RFA (wa pili kushoto), baada ya
kukabidhiwa mbegu bora za Viazi lishe aina ya Kabode kwa ajili ya
kuzipanda kwenye shamba darasa katika kata hiyo wilayani humo leo.
Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi wa COSTECH ambaye ni Ofisa Mwandamizi wa COSTECH, Audax Mutagwa, akimkabidhi mbegu za mihogo, Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmshauri ya Wilaya ya Uyui, Hadija Makuwani kwa ajili ya
kupanda katika shamba darasa katika Kijiji cha Isikizya wilayani humo.
Wengine ni wakulima wa kijiji hicho.
Wanakikundi cha Mapambano katika Kijiji cha Iberamilundi wakifurahi mbegu bora ya mihogo baada ya kukabidhiwa.
Wakulima wa Kijiji cha Isikizya wakiwa kwenye uzinduzi wa shamba darasa.
Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi wa
COSTECH ambaye ni Ofisa Mwandamizi wa COSTECH, Audax Mutagwa,
akizungumza na wakulima na wakulima wa Kijiji cha Isikizya (hawapo
pichani). Kutoka kushoto ni Mshauri wa Jukwaa la Bioteknolojia kwa
Maendeleo ya Kilimo (OFAB), Dk.Nicholaus Nyange na Mtafiti kutoka
COSTECH, Bestina Daniel.
Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya
Uyui, Hadija Makuwani akizungumza na wakulima kabla ya kuzindua shamba
darasa la mbegu ya mihogo katika Kijiji cha Isikizya.
Wakulima wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Mkulima, Gervas Fungameza akiuliza swali.
Mkulima Said Mirambo wa Kijiji cha Isikizya akiuliza swali.
Mtafiti wa mazao ya mizizi kutoka
Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha ARI-Maruku mkoani Kagera, Jojianas
Kibura, akielekeza ubora wa mbegu ya mihogo aina ya mkombozi jinsi ya
kuipanda
Mkurugenzi Mtendaji wa wilaya hiyo, Hadija Makuwani akizindua shamba darasa hilo kwa kupanda mbegu ya mihogo.
Diwani wa Kata ya Isikizya akipanda mbegu hiyo.
Kaimu Ofisa Kilimo wa Wilaya ya
Uyui, Hamphrey Kilua akizungumza na wanakikundi cha Mapambano kabla ya
kuzindua shamba la Viazi lishe katika Kijiji cha Iberamilundi.
Wanakikundi cha Iberamilundi wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Mtafiti wa mazao ya mizizi kutoka
Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha ARI-Maruku mkoani Kagera, Jojianas
Kibura, akiwaelekeza wanakikundi cha Mapambano cha Kijiji cha
Iberamilundi namna ya kupanda mbegu ya mihogo katika shamba darasa.
Mwenyekiti wa kikundi hicho, Jumanne Said Mnubi
akipanda mbegu hiyo.
Katibu wa Kikundi hicho, Clementina Nyamizi akipanda
mbegu katika shamba darasa.
Wanakikundi cha Upendo cha Kata ya Magiri wakiwa na mbegu zao mkononi za Viazi lishe
Na Dotto Mwaibale, Uyui Tabora
HALMASHAURI ya Wilaya ya Uyui mkoani
Tabora imezipokea kwa mikono miwili mbegu bora za mahindi aina ya Wema,
Viazi lishe na mihogo zilizotolewa na Tume ya Taifa ya Sayansi na
Teknolojia (COSTECH) kwa kushirikiana na Jukwaa la Bioteknolojia kwa
Maendeleo ya Kilimo (OFAB)
Mbegu hizo zimetolewa katika vijiji
vitano vya wilaya hiyo kwa ajili ya kuanzisha mashamba darasa ambavyo
vimetajwa kuwa ni kijiji cha Isikizya kilichopo Kata ya Isikizya ambacho
kitakuwa na shamba darasa la zao la mihogo, Ibelamilundi ambacho pia
zao lake ni mihogo, Kijiji cha Kigwa ambacho zao lake ni Viazi lishe,
Igalula ambacho kitapandwa mahindi na Magiri ambacho kitakuwa na shamba
darasa la zao la Viazi lishe.
Akizungumza wakati wa kupokea mbegu hizo
Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya hiyo, Hadija Makuwani alisema wao kama
wilaya wamezipokea mbegu hizo kwa mikono miwili na watazifanyia kazi ili
waweze kupata mazao yenye tija.
"Kwa kweli tunawashukuru sana COSTECH na
OFAB kwa kutuletea mbegu hizi kwani tuna imani zitatuondelea changamoto
ya kupata mazao machache kutokana na kutumia mbegu za kienyeji
zilizozoeleka kwa wakulima wetu" alisema Makuwani.
Makuwani alisema hata yeye kwa kuwa ni
mkulima anaomba apatiwe mbegu hizo ili akazipande kwenye shamba lake ili
hapo baadaye nawe aweze kusambaza mbegu hiyo.
Diwani wa Kata ya Isikizya, Ally Mtelela
alisema mbegu hizo zitazidisha ari kwa wakulima hao na wataondokana na
kilimo kisicho na tija ambacho walikuwa wakitumia mbegu ambazo zilikuwa
zikishambuliwa na magonjwa.
Mtafiti wa mazao ya mizizi kutoka Kituo
cha Utafiti wa Kilimo cha ARI-Maruku mkoani Kagera, Jojianas Kibura
aliwaambia wakulima hao kuwa hekta moja ya mihogo iwapo watalipa kwa
kufuata ushauri wa wataalamu wataweza kupata tani 25 hadi 32 na kwa zao
la viazilishe watapata tani 7 hadi 9 kwa hekta moja.
Alisema matokeo hayo watayapata endapo
watafuata kanuni bora za kilimo cha mazao hayo kwa kuzingatia nafasi
kati ya mche na mche na mstari kwa mstari na matumizi ya mbolea hivyo
wataweza kuongeza uzalishaji zaidi tofauti na sasa ambapo kwenye hekta
moja ya mihogo wanapata tani nane hadi kumi wakati kwenye Viazi lishe
wanapata tani moja hadi tatu.
Kibura alisema Viazi lishe hivyo aina ya
kabode vina vitamini A ambavyo ni muhimu kwa watoto kwa lishe na rangi
yake ni vya njano na vinaisaidia serikali kuacha kutumia matone ya
vitamini A badala yake mtu akivila anapata vitamini hiyo moja kwa moja.
Akizungumzia kuhusu mbegu Mwakilishi wa
Kaimu Mkurugenzi wa COSTECH ambaye ni Ofisa Mwandamizi wa COSTECH, Audax
Mutagwa, alisema mbegu hizo ya mihogo aina ya Mkombozi imefanyiwa
utafiti na kuonekana ina uwezo mkubwa wa kustahimili magonjwa kama ya
batobato kali na michirizi ya kahawia ambayo imekuwa ikiwapatia hasara
kubwa wakulima na ya mahindi ikistahimili hali ya ukame na kutoa mazao
mengi.
Mutagwa aliwaomba wakulima hao kuyatunza
mashamba hayo ambayo yamegharimu fedha nyingi hadi kukamilika kwake
hivyo wayaendeleze kwa ajili ya kuja kutoa matunda kwa wakulima wa
wilaya hiyo na kupata chakula cha kutosha na ziada kuuza.
Mkulima Clementina Nyamizi wa Kijiji cha
Iberamilundi ambaye ni Katibu wa Kikundi cha Mapambano alisema
wanaamini mbegu hizo zitawatoa katika umasikini na kuwa watazitunza na
kuzilinda na wataachana kabisa na mbegu za kienyeji walizokuwa
wakizitumia zamani.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712727062)
0 comments:
Post a Comment