Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Muhuridede wilayani Uyui wakifuatilia 
mafunzo ya unynyuziaji wa dawa sahihi za kuua wadudu katika zao la pamba
 yaliyokuwa yakiendeshwa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey mwanri katika 
ziara yake katika maeneo mbalimali ya kuokoa zao hilo.
RS TABORA
12 MARCH 2018
WAKULIMA wa Pamba na mazao mengine Mkoani Tabora wametakiwa kutumia fedha zinazotokana na  mauzo ya mazao yao katika shughuli za kuendeleza  familia zao na kupanua shughuli zao za kilimo ili waweze kuondokana na kilimo cha kizamani na waendeshe shughuli zao kisasa.
Kauli hiyo 
imetolewa jana Wilayani uyui na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri 
wkati wa ziara yake katika maeneo mbalimbali mkoani humo kuelimisha 
wakulima wa pamba juu ya unyunyuziaji sahihi wa zao hilo kwa ajili uya 
kuua wadudu waharibifu.
Alisema 
fedha wanazozipata ni vema wakazitumia kwa matumizi sahihi na mahitaji 
ya lazima badala ya kutumia fedha hizo kwa shughuli ambazo sio za msingi
 kama vile starehe, ulevi, shughuli za ushirikina ambazo kwa kiasi 
kikubwa zinawarudisha nyuma kimaendeleo na kuzifanya familia zao 
kuendelea kuishi maisha duni.
"Ndugu 
zangu najua mtapata fedha nyingi kwa kuwa mumelima pamba kwa wingi na 
vizuri ...naomba tumieni fedha mtakazopata katika kujenga nyumba nzuri, 
kula vizuri, kusomesha watoto wenu, kuvaa nguo nzuri na ikibidi kununua 
vyombo vya usafiri kwa ajili ya matumizi ya familia zenu" alisema 
Mwanri.
Alisema 
kuwa fedha watakazopata ni vema pia zikawasaidia katika kuboresha kilimo
 chao na kukitoa katika hali ya kilimo cha mazoea cha kuzalisha mazao 
kwa ajili ya matumizi ya kila siku na kuingia katika uzalishaji ambao 
unampa mkulima ziada ambayo ndio itakayomwezesha kupata maendeleo.
"Tukitaka 
kufanikiwa ndugu zangu wakulima wangu wazuri ambao ninawapenda ni 
kulenga katika uzalishaji unaowapa ziada...bila ziada hakuna 
maendeleo...ziada ndio itawasaidia kuwa na fedha kwa ajili ya kununua 
mabati, ziada ndio itawasaidia kununulia simenti na vitu vingine kwa 
ajili ya kuboresha maisha yenu" alisema Mkuu huyo wa Mkoa.
Mkuu huyo 
wa Mkoa alisema ni jukumu la viongozi kuwatahadharisha wananchi ikiwemo 
wakulima kuwa na matumizi shaihi ya mapatao ya ili kujiletea maendeleo 
yao binafsi na Taifa kwa ujumla.
Naye 
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tabora-Uyui Said Ntahondi 
aliwataka wanaume kuacha kutumia fedha wanazozipata kutokana na mauzo ya
 mazao bila kuwashirikisha wake zao kwa kuwa kufanya hivyo mara nyingine
 fedha zinaishia katika matumizi yasiyo sahihi.
Alisema 
pindi wanapopata fedha ni vema wakaweka vikao vya kifamilia ili kubaini 
vipaumbele vya matumizi ya fedha walizopata kabla ya kuanza kuzitumia 
ili ziweze kunufainisha watu wote katika familia.
Naye 
Mkulima kutoka Kijiji cha Muhuridede wilayani Uyui Helena Augustino 
aliwaomba wanaume kuzingatia ushauri wa Mkuu wa Mkoa wa Tabora wa 
kupenda kukimbilia mijini pindi wanapokea fedha za mauzo na kujikuta 
zikimalizika katika anasa na starehe huko familia ikiendelea kutabika.
Alisema 
inapotea hali hiyo wanaopata shida ni wanawake na watoto ambao kwa kiasi
 kikubwa ndio wanaoshiriki katika shughuli za shamba
MWISHO
mwisho
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
0 comments:
Post a Comment