Home » » MKUU WA MKOA WA TABORA AHIMIZA WANANCHI KUWAFICHUA WAGENI KWENYE ZOEZI LA USAJILI VITAMBULISHO VYA TAIFA

MKUU WA MKOA WA TABORA AHIMIZA WANANCHI KUWAFICHUA WAGENI KWENYE ZOEZI LA USAJILI VITAMBULISHO VYA TAIFA

 
Mkuu wa mkoa wa Tabora Mhe. Agrey Mwandri akiongea na wananchi wa kijiji cha Ussoke Mlimani kushiriki zoezi la usajili wa Vitambulisho vya Taifa. Kushoto ni Maafisa wa NIDA Emiliana Temu na Grace Msacky.


Mwenyekiti wa kijiji cha Ussoke Kilimani Bw. Jackson Kitwe (kushoto/mwenye kofia) Akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa Mhe. Agrey Mwandri na Mkuu wa Wilaya ya Urambo Mhe. Anjelina George Kwingwa walipofanya ziara kijijini hapo.  
  Afisa Usajili mkoa wa Tabora Bi Grace Msacky akiwa na Mkuu wa Mkoa Mhe. Agrey Mwandri wakihamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi wakati wa zoezi la Usajili linaloendelea Wilayani humo.
 
 Wananchi wa kata ya Mpela wakiwa wamekusanyika kwenye ofisi za Kata ili kuhojiwa na Maafisa uhamiaji ikiwa ni sehemu ya kukamilisha Usajili Vitambulisho vya Taifa unaoendelea Wilayani humo.

Maelekezo hayo ameyatoa wakati alipofanya ziara ya kutembelea maendeleo ya zoezi la Usajili unaoendelea Wilaya ya Urambo kijiji cha Ussoke Kilimani.
“wananchi ndio mnaokaa na hawa watu; mnaifahamu vizuri historia yao na ujaji waoo kwenye maeneo yenu; msikae kimya na kuwaruhusu kujipenyeza kwenye hizi zoezi; tafadhali muisaidie Serikali” alihimiza.
Akimkaribisha Mkuu wa Mkoa huo kuzungumza na wananchi; Mkuu wa Wilaya ya Urambo Mhe. Anjelina Kwinga amesema zoezi la NIDA halina lengo la kuwabagua wananchi isipokuwa kila mtu anayeishi Wilayani humo atapata fursa ya kusajiliwa na kupata Kitambulisho kulingana na hadhi yake (Raia, Mgeni Mkaazi au Mkimbizi).
Aidha amewataka viongozi wote wa Kata na Vijiji kutoa ushirikiano kwa NIDA na kuwasaidia wananchi kusajiliwa pindi zoezi linapofika kwenye maeneo yao.


0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited : |
Copyright © 2012. Tabora Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za mikoa