NA TIGANYA VINCENT
RS-TABORA
13 February 2018
SERIKALI
ya Mkoa wa Tabora imesema mafunzo ambayo yanayotolewa kwa wafugaji wa
nyuki hapa nchini yamesaidia kuongezeka uzalishaji wa mazao ya asali na
hivyo kuwepo na uwekezaji katika biashara ya mazao ya nyuki.
Hatua
hiyo imetokana kuwepo kwa soko kubwa dunia la mazao ya nyuki ambalo
limefanya kuwepo na chachu kufungua mianya ya wafugaji na
wafanyabiashara kutaka kujifunza juu ya uzalishaji unaoazingatia ubora
na unaokubalika kitaifa na kimataifa.
Kauli
hiyo jana na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Nathilis Linuma wakati
akifungua mafunzo ya siku tano ya wafanyabiashara wa biadha zinazotokana
na nyuki katika Chuo cha Nyuki na kuwashirikisha washiriki kutoka
Mwanza, Simiyu na wenyeji.
Linuma alisema takwimu zinaonesha
kuwa uzalishaji wa mazao ya nyuki hususani asali na nta unaongezeka
kutoka tani 9,000 za asali kwa mavuno ya mwaka 2012 hadi tani 34,000
za asali kwa mavuno ya mwaka 2016 .
Aliongeza
kwa mauzo ya nje ya asali yalikuwa tani 103.8 mwaka 2012 na kufikia
tani 259.9 kwa mwaka 2016 yenye thamani ya Shilingi 2,257,410,880.
Linuma
alisema kwa upande wa nta mwaka 2012 iliuzwa tani 277 ambapo hakukuwa
na ongezeko na kasi kilichouzwa mwaka 2016 ilikuwa ni tani 251.9 yenye
thamani ya Shilingi 4,549,643,832.
Kaimu
Katibu Tawaka huyo wa Mkoa alisema kuwa ongezeko hilo la uzalishaji
linatokana na mwitikio wa wananchi kupata elimu ya ufugaji wa kisasa na
kuwekeza katika mashamba ya ufugaji nyuki nchini.
Aidha
alisema kuwa ili uzalishaji uendelee kuongezeka ni vema wafugaji na
jamii wakaendelea kuhakikisha wanatunza mazingira na kupanda miti kwa
wingi ili nyuki wapate chakula cha kuzalishia asali na pia wasaidia
mimea mashambani.
Kwa upande wa
Mkuu wa Chuo cha Ufugaji Nyuki Tabora Semu Daud alisema wameamua kutoa
mafunzo ya muda mfupi kwa wafugaji mbalimbali hapa nchini kwa lengo la
kuhakikisha kuwa bidhaa wanazozalisha zinakubalika ndani na nje ya
Tanzania.
Alisema
wanashirikiana na Shirika la Viwango Tanzania(TBS), Mamlaka ya Chakula
na Dawa(TFDA) ili kuhakikisha mazao yanayozalishwa yanakuwa yanaviwango
viwango vinakubalika na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania
(TanTrade) kwa ajili ya kuwatafutia masoko ndani na nje ya Tanzania.
Tanzania
ina maeneo makubwa ambayo ufugaji nyuki unatekelezwa, baadhi ya mikoa
hiyo ni pamoja na Dodoma, Singida, Shinyanga, Tabora, Kigoma, Simiyu,
Mwanza, Katavi na Kagera ambayo inapitiwa na barabara iendayo Burundi,
Rwanda na Uganda, barabara hii ni fursa kwa mazao ya nyuki kuelekea soko
la nchi jirani.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment