MIAKA 25 YA VYAMA VINGI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Michael Eneza

 • Jini limerudi kwenye chupa, au Magufuli atashindwa?
WAKATI wa mjadala wa kuingia au kukataa kuingia mfumo wa vyama vingi mwaka 1991, aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, hayati Rashidi Mfaume Kawawa, alisema kuwa hatuna budi kuingia katika mfumo mpya kwani utii wa jadi kwa Chama Cha
Mapinduzi haupo tena miongoni mwa Watanzania walio wengi.


Rashidi Mfaume Kawawa.
Alitumia nahau ya utamaduni wa Kiswahili kusema “jini limetoka kwenye chupa, huwezi kulirudisha,’ akichukulia utii wa watu kama kitu kikubwa, kikishabadilika mandhari yake, mwelekeo wake, basi.
Ni wazi kuwa awamu ya tano haijikiti katika hisia hiyo, ila ya utii kwa chama tawala, sivyo?
Mwaka mmoja baada ya kuingia madarakani kwa awamu ya tano, ni wazi kuwa hakuna mfumo wa vyama vingi unaoendelea bali ule wa chama kimoja, kwani hali hiyo inaonekana kuwa ndiyo inayofaa kuleta nidhamu serikalini, na kurahisisha kupitisha maamuzi.
Eneo lake la kwanza ni kuzuia wabunge kuwasiliana moja kwa moja na wananchi kupitia vyama vyao vya siasa, ila kama wanafanya kazi walizopangiwa na dola, yaani kusimamia miradi ya maendeleo, na kujadili hayo tu.
Mengine zaidi ya hapo, yanayotokana na ajenda za upinzani, yanafuatiliwa kwa karibu kama hisia za uchochezi.
Swali linakuja kama hali hii ni kielelezo cha jinsi jamii ilivyosimama na kuridhia kurudi katika mfumo wa chama kimoja, kwani hata wakati ule wapo wengi tu ambao hawakuwa na imani na mfumo wa vyama vingi.
Ikiwa mazingira hayo ya kisaikolojia ni sahihi, kuwa mfumo au mwelekeo wa dola hauna tatizo uwe ni wa chama kimoja au vyama vingi, itakuwa ni utamaduni wa Mtanzania ulikuwa haujabadilika, hivyo mfumo wa vyama vingi ungekuwa ni raha ya aina fulani, au ukimnukuu Mwalimu vibaya, ni ‘ulevi tu.’ Ndivyo alivyosema mwanamapinduzi wa Russia, Vladimir Lenin, kukataa vyama.
Kwa upande mwingine, zipo nadharia za maendeleo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii kwa jumla ambayo ni pamoja na mabadiliko ya mpangilio wa fikra za watu kutoka mfumo wa chama kimoja kwenda mfumo wa vyama vingi.
Nyakati zile za awali jamii ilikuwa inafikiria kijumlajumla, kwa mfano hatari ya Tanganyika kutawaliwa na mabeberu n a viongozi wapenda mabadiliko (wapinga mifumo ya kikoloni na kibepari) kuuawa, nchi kupinduliwa.
Ni hisia hiyo iliyoainisha umuhimu wa kumuunga mkono Mwalimu kwa ajili ya uhai wa taifa, na siyo kwa sababu kitamaduni hatujui upinzani, kuheshimu wazee.
Ina maana kuwa kwa mfumo huo wa hisia, kuunga mkono serikali kama jambo la lazima kwa uhai wa taifa, hisia hizo ziliambatanana na kipindi halisi cha woga kuhusu hatma ya taifa,, ambayo kwa upande mwingine iliendana na uchanga wa taifa na nafasi maalum ya Mwalimu Nyerere katika hisia za Watanzania.
Pale ambapo vigezo vyote hivyo havipo, ni kwa mantiki gani ambapo awamu ya tano inarudisha nidhamu ya chama kimoja, iwe ni kosa kuongea na kujumuisha watu kiupinzani, na huku vyama siyo tu vimeandikishwa bali vina wawakilishi wengi tu bungeni? Iweje wabunge na hasa wa chama tawala wawe radhi kwa hali hiyo, wapitishe kanuni kutotangazwa ila kwa mbinde shughuli za Bunge?
Ukianza kutafakari ridhaa ya wabunge wa chama tawala kwa hali iliyopo unaanza kupata majibu kuhusu mifumo ya hisia na malengo au mikakati ya kisiasa ya kurudisha utawala wa chama kimoja, kupunguza upinzani kwa kiwango kinachoridhisha kufifisha sauti yake, Siyo tena hisia ya kitaifa ya hatari ya kuwepo migawanyiko kati yetu, kuwa baadhi wanaweza kununuliwa na ubeberu wakawa mawakala wa kuvuruga nchi, livyosema Nyerere wakati akitetea sheria ya kuweka watu kizuizini (Preventive Detention Act) ya mwaka 1962.
Alikuwa akifungua kampasi ya Mlimani ya Chuo Kikuu cha Afrika Mashariki kwa upande wa Dar es Salaam, Aprili 1964, kwamba ilikuwa lazima kabisa.
Kwa vigezo hivyo, siyo rahisi kwa chama tawala kutumia fikra ya jumla kuhusu umoja wa nchi na hatari zinazoikabili kutetea kurudisha mfumo wa chama kimoja katika utendaji wa kila siku.
Na isitoshe, urudishaji huo hauwezi kufikia mahali ambapo chaguzi halisi za vyama vingi zinaondolewa kabisa au uchaguzi unafutwa endapo matokeo ni hasi kwa utawala, jambo ambalo limewezekana kwa sehemu ndogo ya nchi isiyojitegemea.
Ingekuwa ni dola ya Visiwani yenye jukumu la kulinda maamuzi hayo isingefanikiwa au ingehitaji machafuko kama Burundi, ambayo ina maana kuwa hali hiyo si rahisi Bara.
Kinachoonekana katika juhudi hizo ni kuwa kulikuwa na ulazima wa kurudisha nidhamu katika utendaji serikalini na mashirika ya kiserikali, na maeneo mengine ya maisha ya nchi kwa jumla, kwa mfano katika kampeni dhidi ya madawa ya kulevya, au viroba.
Ina maana kuwa chama tawala kinaona kuwa vizuizi vyote hivi ni lazima ili kunusuru hali ya mkanganyiko kuhusu uongozi na maadili kwa jumla, iliyofikisha chama tawala katika hatari ya kunyang’anywa dola na upinzani. Inaashiria hisia ya kujilinda, kwa kuhofu upinzani, na siyo mshikamano halisi wa kitaifa kutaka ‘demokrasia ya chama kimoja.’
Tatizo hapa ni mazingira ambako mwafaka huu wa kihisia ndani ya chama tawala, kutoa sehemu ya uhuru wake kwa ‘Leviathan,’ mtawala madhubuti, ili anyooashe mambo yao pale ambapo wameshindwa kuyaendesha vyema kidemokrasia, yataendelea kudumu.
Yako maeneo mawili ya kuridhia hali iliyopo kwa sasa, moja ikiwa ni ndani ya chama tawala na nyingine ikiwa ni ndani ya jamii kwa upana wake, kwa maana kuwa hata upinzani kwa kiwango fulani unazuiliwa katika mielekeo yake na inachojua kinatawala hisia za watu. Wanataka mabadiliko, na hivyo serikali iliyopo inapewa muda ili ifuzu.
Kwa upande wa chama tawala, hali hii ya ‘demokrasia ya chama kimoja’ inaweza kuendelea kwa kipindi chochote mradi tishio la upinzani bado lipo, au tuseme kuna mtazamio kuwa baada ya kipindi cha mpito imani ya wananchi itakuwa imerejeshwa tena kwa CCM.
Uhuru hautaashiria tena uwezekano wa kuondolewa chama tawala, lakini kuna upande wa pili, kuwa sehemu ya chama tawala inaanza kuona kuwa uhuru ndiyo jambo muhimu, na kama inahitaji upinzani uingie madarkani ili uhuru uhakikishwe, ni vyema.
Kwa njia hiyo, utawala uliopo kutegemea mshikamano chama tawala si rahisi.
  CHANZO GAZETI LA NIPASHE

  ZIARA YA MKURUGENZI WA NAMAINGO KUIMARISHA UJASIRIAMALI MIKOANI

  Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
   Mkurugenzi wa Kampuni ya Namaingo Business Agency, Ubwa Ibrahim akiwa katika moja ya ,ya mikoa kukagua na kuimarisha shughuli za Wajasiriamali wanachama wa kampuni hiyo katika mikoa mbalimbali nchini. Tayari hadi leo ameshafanya ziara katika mikoa ya Iringa, Tabora, Kigoma, Manyara, Arusha na Kilimanjaro.

  Mafunzo yanayotolewa na kampuni hiyo kwa wajasiriamali zaidi ya 400,000 nchini ni. ufugaji wa kuku wa chotara, sungura, samaki pamoja na kilimo bishara cha mbogamboga na matunda.

  Pia husaidia kupatika kwa masoko ya bidhaa hizo, pamoja na kuwaunganisha katika taasisi mbalimbali za kifedha ili kupata mikopo kirahisi. Imeandaliwa na Richard Mwaikenda; Kamanda wa Matukio Blog  MA MAGUFULI NA MAMA MAJALIWA WATEMBELEA GEREZA LA MAHABUSU LA TABORA, WATOA ZAWADI KWA WAFUNGWA

  Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
   Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akipokea risala toka kwa Kaimu Mkuu wa
  Magereza Mkoa wa Tabora Mkuu wa gereza SSP Nahman Koko wakati yeye na mke
  wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa walipotembelea Magereza ya mahabusu ya
  Tabora na kutoa zawadi mbalimbali kwa wafungwa mahabusu.
   Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akimkabidhi zawadi  Naibu Mkuu wa
  gereza la Mahabusu Tabora Mrakibu wa Magereza Godliver Makwaruzi  wakati
  yeye na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa walipotembelea Magereza ya
  mahabusu ya Tabora na kutoa zawadi mbalimbali kwa wafungwa na mahabusu leo
  Februari 14, 2017.

  Mke wa Rais Mama Janeth magufuli na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary
  Majaliwa wakiagana na askari magereza bada ya kutembelea Magereza ya
  mahabusu ya Tabora na kutoa zawadi mbalimbali kwa wafungwa na mahabusu leo
  Februari 14, 2017
  NA MWANDISHI MAALUM

  MKE wa Rais Mheshimiwa Mama Janeth Magufuli na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary
  Majaliwa wametembelea Gereza la Mahabusu Tabora na kutoa zawadi mbalimbali
  kwa wafungwa na mahabusu gerezani hapo.

  Wake wa viongozi wametembelea gereza hilo leo (Jumanne, Februari 14, 2017)
  wakiwa katika ziara  mkoani Tabora, ambapo Mama Janeth amesema wameamua
  kuwatembelea wafungwa na mahabusu hao kwa nia ya kuwafariji kwa kuwa wao ni
  sehemu ya jamii.

  “Vitabu vitakatifu vinasema kwamba ukiwasaidia watu wenye mahitaji utakuwa
  umetoa sadaka kubwa kwa Mwenyezi Mungu, hivyo tumeamua kuja kutembelea
   wafungwa na mahabusi kwenye gereza hili na kuwapa zawadi kwa kuwa nanyi
  mnahitaji faraja,” amesema.

  Amesema wameamua kwenda kuwaona wafungwa na mahabusu hao kwa lengo la
  kuwafariji na kuwatia moyo kwa sababu wanaimani kwamba wakitoka watakuwa
  raia wema na hayo wanayopitia ni sehemu ya kufanya marekebisho ya tabia.

  “Ni siku kubwa kwangu, nimejifunza mengi baada ya kufika hapa. Kitendo cha
  kwenda kuwaona wenye mahitaji wakiwemo wagonjwa, wafungwa ni jambo jema
  tunaamini hizi zawadi tulizozitoa zitawasaidia kwa sababu tunajua
  mnamahitaji mengi,” amesema.

  Katika gereza hilo wake hao wa viongozi wamekabidhi zawadi mbalimbali kwa
  wafungwa na mahabusu, ambapo mwakilishi wa wafungwa hao Deo Kitave
  aliwashukuru kwa niaba ya wenzake. “Tunawashukuru kwa kutukumbuka,
  tunamuomba Mwenyezi Mungu muendelee kuwa na moyo huo,”.

  TTCL YATOA MSAADA WA VIFAA VYA MAABARA KWA SHULE ZA SEKONDARI TABORA VYENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI SABA

  Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

  Mkuu wa mkoa wa Tabora Bw.Aggrey Mwanry akipokea msaada wa vifaa hivyo vya maabara ya Sayansi kutoka kwa Meneja wa TTCL tawi la Tabora Bw.James Mlaguzi,vifaa hivyo vinathamani ya shilingi milioni saba.

  Meneja wa TTCL tawi la Tabora Bw.James Mlaguzi akisoma taarifa fupi ya kukabidhi msaada huo wa vifaa vya maabara vilivyogharimu jumla ya shilingi milioni saba.
  Meneja wa TTCL tawi la Tabora Bw.James Mlaguzi akikabidhi taarifa aliyoisoma wakati wa kukabidhi vifaa hivyo vya maabara ya Sayansi kwa Shule za Sekondari kwa Mkuu wa mkoa wa Tabora Bw.Aggrey Mwanry.
  Baadhi ya maafisa wa Kampuni ya Simu Tanzania TTCL katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule za Sekondari ya Tabora Wavulana na Wasichana nje ya Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Tabora baada ya hafla fupi ya TTCL kukabidhi msaada wa vifaa vya Maabara ya Sayansi kwa Shule za Sekondari za mkoa wa Tabora.


  Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Tabora Wasichana wakiwa wamebeba masanduku ya vifaa vya maabara vilivyotolewa msaada na Kampuni ya Simu Tanzania TTCL

  Baadhi ya maafisa wa TTCL wakati wa hafla fupi ya kukabidhi vifaa vya maabara ya sayansi vilivyokabidhiwa na Kampuni hiyo ya simu Tanzania.

  Askari 9 JKT watuhumiwa kuua mwananchi

  Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


  MKAZI wa Kata ya Chemchem katika Manispaa ya Tabora, Asha Kayamba amemuonba Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) na vyombo vya ulinzi na usalama vimsaidie ili askari wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) waliompiga mwanawe na kumsababishia kifo wachukuliwe hatua za kisheria.
  Katika barua yake, amemlalamikia Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kuwaachilia askari tisa wa Kikosi cha 823 JKT Msange kwa madai ya kukosekana ushahidi.
  Asha katika barua hiyo ya Desemba 19, 2015, alisema anasikitika kuona haki yake inapokonywa na kauli ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwamba kijana wake Omary Zuberi Shaban (19) ambaye sasa ni marehemu, aliuawa na wananchi wenye hasira.
  “Kwa kweli nilipatwa na mshtuko mkubwa sana baada ya kuona haki yangu inapokonywa kwa kisingizio cha mtoto wangu kuuawa na watu wenye hasira,” alieleza Asha katika barua yake kwa DPP.
  Alibainisha kuwa mwanawe alishambuliwa na wanajeshi hao (majina na vyeo vyao tunayahifadhi) mchana na wala wananchi hawakuhusika katika tukio hilo kwani wao walikuwa ni watazamaji tu.
  Alisema mwanaye alipigwa na askari hao Septemba 10, mwaka jana na alilazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kitete kwa siku nne hadi alipoaga dunia Septemba 13, 2016 saa tano usiku.
  Barua hiyo ilieleza kuwa Polisi ilifanya upelelezi wa tukio hilo na kuwatia nguvuni watuhumiwa tisa wakati mama wa marehemu, Regina Masuva, kijana aliyenusurika Zuberi Haruna, Mwaka Zuberi (mama mzazi wa Zuberi) na watu wengine walitoa maelezo kuhusu tukio hilo.
  Alifafanua kuwa Septemba 20, 2016 watuhumiwa wa mauaji ya mwanawe ambao ni askari tisa wa Kikosi cha 823 Msange JKT walifikishwa mahakamani na kusomewa mashtaka na Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Samson Kabigi mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Agatha Chugulu.
  “Baada ya kusomewa mashitaka hayo, kesi hiyo ilipangwa kutajwa Oktoba 13, 2016 na Oktoba 28, 2016. Lakini siku hiyo watuhumiwa hao hawakufikishwa mahakamani.
  “Nilipohoji kwa nini nilijibiwa kuwa walifanya fujo ndani ya mahabusu ya gereza la Uyui mjini Tabora, jambo lililowafanya wapewe adhabu hivyo hawataweza kufika,” alieleza mama huyo katika barua hiyo.
  Alisema shauri hilo lilipangwa kutajwa Novemba 10, mwaka huu, nilipofika siku hiyo watuhumiwa walikuwepo mahakamani ambapo kesi yao ilipangwa kutajwa tena tarehe 24 Novemba, mwaka huu.
  Alisema kuwa utata ndio ulianzia hapo.
  Alidai kuwa kabla ya kufika tarehe hiyo, watuhumiwa wote tisa walionekana mtaani jambo ambalo lilimpa mshituko mkubwa na kufanya afuatilie mahakamani, Polisi na Ofisi ya Mwanasheria wa Serikali mjini Tabora bila kupata majibu muafaka.
  Alidai alipofika Ofisi ya Mwanasheria wa Serikali, alikutana na ofisa aliyemtaja kwa majina ya Jackson Bulashi ambaye alidai kuwa alimjibu kwamba watuhumiwa hao waliokuwa wanakabiliwa na shauri la mauaji, wameachiwa kwa kuwa hakuna ushahidi wa kujitosheleza.
   CHANZO GAZETI LA HABARI LEO

  KUWAIT YAIPATIA TANZANIA MKOPO NAFUU WA UJENZI WA BARABARA MKOANI TABORA

  Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
  Na Benny Mwaipaja, WFM, Dar es salaam
  Serikali ya Kuwait imeahidi kuipatia Tanzania mkopo wenye masharti nafuu wa dola za Kimarekani milioni 34 sawa na zaidi ya shilingi Bilioni 74.8 kwa ajili ya ujenzi wa barabara yenye urefu wa Kilometa 85 kwa kiwango cha lami kutoka eneo la Chaya hadi Nyahua mkoani Tabora.
  Ahadi hiyo imetolewa Jijini Dar es salaam na mwakilishi wa Balozi wa Kuwait hapa nchini, Bw. Mohammad Rashid Alamiri, aliyeongoza ujumbe kutoka Mfuko wa Maendeleo wa Kuwait, ulipomtembelea na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, ambapo wamejadili masuala mbalimbali ya ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kati ya Tanzania na Kuwait.
  Dkt. Mpango ameushukuru Mfuko wa Maendeleo wa Kuwait (Kuwait Fund) kwa kuipatia Tanzania mkopo  huo wenye masharti nafuu utakaochochea maendeleo kwa Watanzania hususani wanaoishi katika maeneo ambayo barabara itajengwa kwa kuwa watarahisishiwa usafiri na usafirishaji wa bidhaa zao hivyo kukuza uchumi wao binafsi na Taifa kwa ujumla.
  Amesema kuwa kipande hicho cha barabara kutoka Chaya hadi Nyahua, ambacho kiko Barabara Kuu itokayo Dar es salaam kwenda katika mikoa ya Tabora na Kigoma, licha ya umuhimu wake katika kukuza biashara na usafiri na usafirishaji wa abiria na mizigo ikiwemo inayokwenda nchi jirani, ilikuwa haijapata fedha kwa ajili ya ujenzi wake.
  “Riba waliyoiweka mezani kwa mazungumzo ni asilimia 2 lakini nimewaomba waangalie uwezekano wa kuiteremsha walau ifike asilimia 1.5 na wamependekeza kipindi cha kuanza kulipa mkopo kiwe miaka ishirini ijayo lakini nimewaomba wasogeze hadi kufikia miaka 25 kama ilivyo kwa mradi wa Hospitali ya Mnazimmoja” aliongeza Dkt. Mpango
  Dkt. Mpango amesema Serikali ya Kuwait kupitia Mfuko wake huo wa Maendeleo wameonesha nia ya kutoa mkopo wenye masharti nafuu kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa Hospitali ya Mnazi Mmoja iliyoko Visiwani Zanzibar.
  “Nawahakikishia kuwa baada ya muda si mrefu wananchi wa mikoa ya Tabora na Kigoma watarajie kuona mkandarasi akiingia kazini ili kujenga barabara hii muhimu sana kwao na kwa uchumi wa Taifa kwa ujumla” Alisisitiza Dkt. Mpango.
  Ameeleza kuwa ujenzi wa kipande cha barabara hiyo kutoka Chaya hadi Nyahua  unatarajia kugharimu shilingi Bilioni 61 lakini Kuwait haitatoa fedha zote hivyo ameuomba Mfuko huo uangalie uwezekano wa kutoa kiasi hicho chote cha fedha  ili uweze kukamilika mapema.

  Miaka 55 ya Uhuru Jimbo la Igalula linajivunia Mafanikio Makubwa

  Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

  TABORA YASHIKA NAFASI YA 10 S/MSINGI KITAIFA

  Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


  Judith Mhina – Maelezo

  Mkoa wa Tabora umeonyesha maajabu sekta ya Elimu baada ya kushika nafasi 10 kimkoa kitaifa 2016.

  Akiongea kwa niaba ya Afisa Elimu Mkoa wa Tabora Bw Emmanuel Malima alisema: “ Ukiangalia mwenendo wa ufaulu kwa Mkoa ulikuwa hauridhishi tangu 2013 ufaulu ulikuwa wastani wa 34.5 na kushika nafasi ya 25 kitaifa ambayo ni ya mwisho, 2014 ufaulu 42.09 nafasi ya 23 2015 ufaulu 50.5 nafasi ya 25 na 2016  ufaulu 71.35 nafasi ya 10 kitaifa, hii imetupa heshima kubwa baada ya kukaa namba za mwisho kwa miaka mitatu mfululizo”.

  Akidhibitisha juu ya ufaulu huo,  Afisa Elimu Taaluma wa Mkoa Bw Emmanuel Malima alieleza : “Matokeo hayo yametokana na juhudi na ushirikiano katika masuala muhimu yaliyoainishwa na Mpango wa Kuinua Ubora wa Elimu yaani EQUIP- Tanzania, katika kuimarisha utendaji wa waalimu, kuimarisha uongozi wa shule, kuimarisha utendaji wa Elimu katika Wilaya na kuongeza ushiriki wa jamii  kuboresha elimu yaani kujizatiti katika - K4. 

  Aidha, Bw Malima aliyasema hayo wakati wa Warsha ya kuimarisha mawasiliano au utoaji wa taarifa katika sekta ya Elimu chini ya Mpango wa Kuinua Elimu EQUIP Tanzania, yaliyofanyika mwezi Novemba katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo kwa takriban siku 6. Mawasiliano au taarifa hizo zinatoka ngazi ya shule, jamii vijijini kata hadi Wilaya.

  Bw Malima alieleza jinsi K4 zilivyoweza kubadili mazoea ya utendaji katika shule za msingi na kuleta mabadiliko makubwa katika Mkoa mzima wa Tabora ambao katika siku za nyuma Mkoa ulikuwa maarufu sana katika suala zima la elimu.

  Mpango wa Kuinua Elimu Tanzania EQUIP-T ulianzishwa mwaka 2014 na una vipengele vitano ambavyo ni: Kuwawezesha Walimu katika kuimarisha mbinu za stadi za ufundishaji, Kuboresha uongozi wa Walimu wakuu na wasaidizi wao, Kusaidia utendaji wao wa kazi na uongozi wa shule;  Kujenga uwezo wa Maafisa Elimu kuongoza kwa ufanisi, kusimamia elimu na mfumo wake; Kuimarisha Ushiriki wa Jamii  Wazazi na Viongozi wa vijiji na mitaa ili kuleta maendeleo ya shule Elimu ya Kujitegemea; na Kuboresha  mifumo ya ukusanyaji , utumiaji na utoaji wa taarifa za kielimu.


   

  “STOP PREGNATING OUR SCHOOL PUPILS “- AGGREY MWANRY

  Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

   
  Judith Mhina – MAELEZO

  The Regional Commissioner for Tabora Region, Honourable Aggrey Mwanry has urged the region to play their part for ensuring that girls fulfil their education and prevent pregnancy of primary school girls.

  He gave this statement during the opening of Ward Education Officers from Tabora Region at a two day EQUIP workshop held at Urambo District Council.

  Mwanry was very furious about the bad habits of the men who cut off the prosperity dreams of the girls before they finish their education carrier.

   “Girls like boys deserve to realise their dreams,” said Mwanry.

  The pregnancy statistics show that, most of the pupils are under 14 of age for example in Urambo District  in 2014 one pupil got pregnant, 2015, three, 2016, four 4 pupils where by 5 cases in police 2 cases in village education Officer and 1 case on District magistrate.  In Igunga  by 2016, six pupils became pregnant all three cases were reported to police and three in District Magistrate.

  RC was a witness to a case in Sikonge District when they found a girl, not in school because the parents decided the girl was to be married before completing her primary education. The Region including the RC himself and The Regional Defence and Safety Committee decided to fetch the parents. Sadly in the meantime the girl was already pregnant. The parents were sent to court, but in vain as all the family have left for another area.
  “I swear, I will use all my efforts to make sure that, they take the families and relatives to court both who marry the school children,” he stressed.

  Mwanry challenged the participants to increase cooperation between parents and schools. Well-informed parents are a key to the success for girls to attend school and the completion of their education without obstacles. He said that school clubs, especially counsellor or parents will open the eyes of the girls to understand that success in life begins with education.

  -ends-
   
   
  Supported by Tone Multimedia Company Limited : |
  Copyright © 2012. Tabora Yetu - All Rights Reserved
  Designed by Fredy Tony Njeje
  Proudly powered by Blogs za mikoa