Home » » WAFUGAJI ZAIDI YA 3000 NCHINI WAKUTANA LEO KWENYE KONGAMANO LAO IGUNGA TABORA

WAFUGAJI ZAIDI YA 3000 NCHINI WAKUTANA LEO KWENYE KONGAMANO LAO IGUNGA TABORA


  Naibu Katibu Mkuu CCWT Ally Manonga (pichani)

.................................

 Na Victor Makinda, Igunga 

Zaidi  ya wafugaji 3000 na wadau wengine wa sekta hiyo hiyo,  kutoka maeneo mbali mbali nchini, wamekutana wilayani Igunga mkoani Tabora kwa ajili ya kufanya Kongamano kubwa la kujadili mafanikio na changamoto zinazoikabili sekta hiyo. 

Hayo yameelezwa leo mjini Igunga na Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Wafugaji Tanzania (CCWT) Ally Manonga (pichani)

Manonga amesema kuwa serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, imetatua matatizo mengi yaliyokuwa yakiikabili sekta ya ufugaji nchini, zipo changamoto chache zinazoikabili ambazo bado zinaikabili sekta hivyo hivyo kongamano hilo litajadili na kupendekeza utatuzi wa changamoto hizo.

"Matatizo mengi ya wafugaji yametatuliwa, bado yapo machache ambayo pia yanatakiwa kutupiwa jicho ili kuyapatia ufumbuzi wa kudumu". Amesema.

Manonga amesema kuwa katika kongamano hilo watajadili mafanikio, changamoto na namna ya kutatua changamoto zilizosalia.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited : |
Copyright © 2012. Tabora Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za mikoa