Na Tiganya Vincent
RS-Tabora
9 Novemba 2017
SERIKALI
ya Mkoa wa Tabora imesema itakamata mali za Kampuni zilizopewa jukumu
la kusambaza pembejeo kwa ajili ya wakulima wa pamba ambao
watawasambashia hasara wakulima ambao watawasambazia mbegu mbovu za
pamba ambazo hazitaota na dawa ilisoua wadudu.
Kauli
hiyo imetolewa hivi karibuni na Mkuu wa Mkoa wa Tabora wakati wa ziara
yake ya kuwaelimisha wakulima wa pamba katika Wilaya ya Uyui.
Alisema
kuwa hawezi kukubali wakulima wapate hasara na yeye akiwa kiongozi
anayebeba dhamana ya kuhakikisha kuwa anatumia vyombo vyote
vinavyomsaidia na kumshauri katika kulinda maslahi ya umma wakiwemo
wakulima wa pamba.
“Kampuni
itakayo sambaza mbegu ambazo hazioti na dawa ambazo haziui wadudu
nitamkamata yeye na mali zake zote ikiwemo magari na kupiga mahesabu ya
hasara waliyopata wakulima na kisha nitamwaandikia invoice ili aweze
kulipa gharama ya hasara hiyo ndio nitamwachia yeye na mali zao” alisema
Mwanri.
Alisema
kuwa hesabu hiyo itahusu kulipa fedha ambazo mkulima angepata kutokana
na kilo ambazo angezalisha katika eneo lake na kwa kuzingatia bei ya
ununuzi wa pamba wa wakati wa mauzo.
Kwa
upande wa Meneja Mbegu kutoka Kampuni ya Usambazaji Mbegu ya Quoton
Tanzania Limited Phineas Chikaura alimwahakikishia Mkuu huyo wa Mkoa
kuwa aina ya mbegu ni salama na kuwaomba wakulima kutochimba mashimo
marefu wakati wa upandaji wa mbegu za pamba kwa sababu zao hilo halina
nguvu za kusukuma udongo kama yalivyo mazao mengine.
Alisema kuwa wakichimba mashimo marefu upo uwezekano wa mbegu kushindwa kuotoa na kudai kuwa ni mbovu.
Chikaura
aliongeza kuwa pia wakulima hawapaswi kuloweka mbegu za pamba kabla ya
kupanda bali wanapaswa kugonja mvua inyeshe ndio wapande.
Alisema
kuwa kitendo cha kuloweka wakati mwingine usababisha mbegu ishindwe
kuotoa endapo mvua ikichelewa kunyesha katika eneo husika,
0 comments:
Post a Comment