Home » » MAKAMU WA RAIS DK. GHARIB BILAL AFUNGA AWAMU YA KWANZA YA MAANDALIZI YA SENSA YA WATU NA MAKAZI, MKOANI TABORA LEO.

MAKAMU WA RAIS DK. GHARIB BILAL AFUNGA AWAMU YA KWANZA YA MAANDALIZI YA SENSA YA WATU NA MAKAZI, MKOANI TABORA LEO.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifunga kitambaa juu ya ramani ya Tanzania, kuashiria kufunga Awamu ya kwanza ya maandalizi ya Sensa ya watu na makazi iliyofanyika leo Mei 9, 2012, Mkoani Tabora. Zoezi la kuhesabu Sensa ya watu na Makazi inatarajia kuanza Tarehe  26 Mwezi Agosti, mwaka huu.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifunua kitambaa kuashiria kuhakiki Ramani ya iliyoandaliwa kwa zoezi la kuhesabu Sensa ya watu linalotarajia kuanza Tarehe  26 Mwezi Agosti, mwaka huu, wakati alipokuwa akifunga Awamu ya kwanza ya maandalizi ya Sensa ya watu na makazi iliyofanyika leo Mei 9, 2012, mkoani Tabora.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi ya Picha ya Ramani ya Tanzania, kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Ramani Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Vincent Mugaya, baada ya kufunga Awamu ya kwanza ya maandalizi ya sensa ya watu na makazi iliyofanyika leo Mei 9, 2012, Mkoani Tabora.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwahutubia wananchi wa Mkoani Tabora wakati akifunga Awamu ya kwanza ya maandalizi ya sensa ya watu na makazi iliyofanyika leo Mei 9, 2012 katika Uwanja wa Chipukizi mkoani Tabora.
 Makamu akiwasili kwenye uwanja wa chipukizi mkoani tabora kufunga awamu ya kwanza ya maandalizi ya  sensa ya watu na makazi iliyofanyika leo Mei 9, 2012 katika Uwanja wa Chipukizi mkoani Tabora. Picha na Muhidin Sufiani-Ofisi Ya Makamu Wa Rais

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited : |
Copyright © 2012. Tabora Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za mikoa