Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi ya Picha ya Ramani ya Tanzania, kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Ramani Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Vincent Mugaya, baada ya kufunga Awamu ya kwanza ya maandalizi ya sensa ya watu na makazi iliyofanyika jana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akionyeshwa Ramani ya makazi itakayotumika na Makarani katika zoezi la kuhesabu Sensa ya watu na makazi, na kusikiliza maelezo kutoka kwa Kamishna wa Sensa, Hajat Amina Said Mrisho, wakati Makamu alipokuwa akifunga Awamu ya kwanza ya maandalizi ya sensa ya watu na makazi.
Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal akiangalia ramani ya Tanzania inayoonyesha maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya sensa ya watu na makazi itakayofanyika mwezi Agosti leo mjini Tabora wakati wa ufungaji wa awamu ya kwanza ya utengaji wa maeneo ya sensa ya watu na makazi huku akiwataka wananchi kushiriki kikamilifu katika zoezi hilo ambalo litaendeshwa kwa usiri na kuongeza kuwa takwimu zitakazopatikana zitatumika katika shughuli za maendeleo na si vinginevyo.
Mkuu wa kitengo cha ramani kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Vincent Mugaya akitoa ufafanuzi kwa makamu wa rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal kuhusu moja ya ramani inayoonyesha maeneo ya sensa ya watu na makazi 2012 jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal akizungumza jambo na mkuu wa mkoa wa Tabora Bi. Fatma Mwasa wakati wa sherehe za ufungaji wa awamu ya kwanza ya utengaji wa maeneo ya sensa ya watu na makazi katika viwanja vya Chipukizi mkoani Tabora.
Wadau wa sensa ya watu na makazi 2012 Bw. Bakari Kimwanga kutoka gazeti la Mtanzania (kushoto) na Bw. Said Ameir kutoka Ofisi ya taifa ya Takwimu (kulia) wakiwa ndani ya msitu wa tula wilayani Uyui kwenye barabara kuu itokayo mkoani Tabora mara baada ya kukamilika kwa shughuli za ufungaji wa awamu ya kwanza ya utengaji wa maeneo ya sensa ya watu na makazi zilizofanyika kitaifa mkoani humo.
Kijana mmoja ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja akiwa katika viwanja vya Chipukizi mjini Tabora kushuhudia ufungaji wa awamu ya kwanza ya utengaji wa maeneo ya Sensa ya watu na Makazi.
Vijana wa kikosi cha ulinzi wa jadi cha Sungusungu (waliokaa chini) pamoja na wananchi wa mkoa wa Tabora wakifuatilia zoezi la ufungaji wa awamu ya kwanza ya utengaji wa maeneo ya sensa ya watu na makazi mkoani Tabora.Picha na Aron Msigwa -MAELEZO.
0 comments:
Post a Comment