Home » » Lile Tamasha la Ngoma Za Utamaduni na Maonyesho ya Biashara la Mtemi Mirambo ni Mwezi Julai Mkoani Tabora

Lile Tamasha la Ngoma Za Utamaduni na Maonyesho ya Biashara la Mtemi Mirambo ni Mwezi Julai Mkoani Tabora

 Mkurugenzi wa taasisi ya Chief Promotions ambao ni waandaaji wa Tamasha la Mtemi Mirambo,Amon Mkoga akionyesha tangazo la Tamasha hilo.
 Msanii wa Muziki wa Bongo Flava kutoka Kundi la Mabaga Fresh,Jumanne Omar akiimba moja ya nyimbo zake atakazoimba kwenye kusindikiza Tamasha la Mtemi Mirambo linalotajariwa kuanza kufanyika Julai 1-3 mkoani Tabora.
--
TAMASHA la ngoma za utamaduni na maonyesho ya biashara la Mtemi Mirambo linatarajiowa kurindima kuanzia Julai 1-3 kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari Uyui,Mjini Tabora.


Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari - Maelezo jijini Dar es Salaam jana,Mkurugenzi wa taasisi ya Chief Promotions ambao ni waandaaji wa Tamasha hilo,Amon Mkoga amesema kuwa Tamasha hilo linalengo la kuenzi na kuuendeleza utamaduni wa Kitanzania,Hususani makabila ya Mikoa ya Tabora,Shinyanga na Mwanza,ambao ni Wanyamwezi na Wasukuma.


Mkoga aliendela kusema pia Michezo na Maonyesho ya bidhaa zenye asili ya Kitanzania pia zitakuwaepo,kama vile mchezo wa bao,kurusha mishale.bila kusahau kutakuwa na uchomaji wa nyama za aina mbalimbali zitakazokuwepo kwenye Tamasha hilo.


Alisema Ijumaa ya Julai 1 shughuli itaanza saa 4:00 asubuhi hadi saa 8:00 usiku na kuendelea kwa muda huo huo hadi siku ya mwisho wa shindano.Mkurugenzi huyo alizitaja baadhi ya ngoma zitakazokuwemo wakati wa tamasha hilo kuwa ni pamoja na Manyanga,Maswezi,Uyeye,Bagalu,Bagika,Bazuba,Radu na nyinginezo nyingi tu.


Afande Sele na Mabaga Fresh ni kati ya wasanii maarufu wa Bongo Flava walioalikwa kunogesha tamasha hilo.Mgeni Rasmi katika Tamasha hilo anatarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora,Mh. Fatma Mwassa.


Kauli Mbiu katika Tamasha hilo kwa Mwaka huu ni KUSHOKE KUHAYA ikiwa lugha ya Kinyamwezi na yenye maana ya kwamba turudi nyumbani.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited : |
Copyright © 2012. Tabora Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za mikoa