Tamasha la kila mwaka la Mtemi Milambo limezinduliwa leo tarehe 1/6/2012 mkoani Tabora ambapo Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mh. Fatma Mwassa katoa wito kwa wananchi kuuenzi utamaduni wao kwani msahau kwao ni mtumwa.
Tamasha hili linafanyika katika viwanja vya shule ya
Uyui Tabora tarehe 1-2, Juni,2012.
Pichani juu ni Mkuu wa mkoa wa Tabora Mh. Fatma Mwassa akijiandaa kurusha mshale juu kama ishara ya uzinduzi rasmi wa Tamasha hilo. Pembeni yake kulia ni Chief Promotions MD Bw. Amon Mkoga.
Tamasha hili linadhaminiwa na TBL kupitia bia ya Balimi,Airtel, Swiss Cooperation, TTB, Channel Ten, Michuzi Blog na Magic FM.
0 comments:
Post a Comment