Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Kazi zikiwa zinaendelea
Mbunge Gulamani
Mbunge
wa Jimbo la Manonga wilayani Igunga Mkoani Tabora Bwn.Seif Khamis
Gulamali (CCM) ameanza kazi za kuwatumikia wananchi wake kwa kushiriki
ujenzi wa wa vyoo pamoja na kuziba mabwawa yaliyoharibiwa vibaya na
mvua.
Gulamali ameziba Bwawa la Maguliati katika kata ya Ziba na kutengeneza mitaro ya maji kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji wa zao la mpunga linalotegemewa na wakazi zaidi ya 600 katika kata ya Choma, pamoja na kushiriki ujenzi wa choo katika shule ya msingi Njia panda kata ya Nkinga.
Mbunge huyo aliyeshinda katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana kwa kura 31,485 sawa na asilimia 67.65% alianza kwa kuwashukuru wananchi wake kwa kuzunguka katika kata zote 19 na kuanzisha ligi ya mpira katika vijiji 68 na kutoa jezi pamoja na mipira kwa kila kijiji.
Aidha Gulamali amewaomba wananchi wake kuonyesha ushirikianio wa hali ya juu ili aweze kutekeleza vyema kazi waliyomtuma ya uwakilishi na watarajie mabadiliko na maendeleo makubwa katika jimbo lao.

Na Tabora yetu
0 comments:
Post a Comment