Na Tiganya Vincent
RS_TABORA
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli kesho
tarehe 23 Julai 2017 ,anatarajiwa kufanya ziara ya siku mbili mkoani
hapa kwa ajili ya uzinduzi wa miradi ya mbalimbali ya maendeleo.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana Ofisi kwake Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bw.
Aggrey Mwanri alisema Mhe. Rais Dkt.Magufuli atawasili mkoani Tabora
akitokea Kigoma ambapo wanatarajia kumpokea katika Wilaya ya Kaliua siku
ya Jumapili .
Alisema
kuwa mara baada ya kuwasili Wilayani Kaliua kuzindua uzinduzi wa
barabara kutoka Kaliua hadi Kazilambwa na baadaye atapata fursa ya
kuwahutubia wananchi.
Bw.
Mwanri aliongeza kuwa akiwa njiani kuelekea Tabora Mhe Rais Magufuli
atazinduza barabara ya Urambo hadi Tabora siku hiyo hiyo na ambapo pia
atawahutubia wakazi wa Urambo na kisha kuelekea Tabora.
Alisema
kuwa siku ya Jumatatu Rais ataweka Jiwe la Msingi ujenzi wa mradi wa
maji kutoka Ziwa Victoria kuja katika miji ya Nzega , Igunga na Tabora
na baadae kuzindua upanuzi na ukarabati wa njia za kurikia Ndege katika
Uwanja wa Tabora.
Mkuu
huyo wa Mkoa wa Tabora aliongeza kuwa siku hiyo hiyo ,Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania atazindua barabara ya Tabora hadi Nzega na ile
ya Tabora hadi Nyahua na mchana atawahutubia wakazi wa Tabora katika
Viwanja vya Chipukizi.
Alisema
ujio wa Rais Magufuli kwa wakazi wa Mkoa wa Tabora ni sawa na usemi
usemao Mgeni Njoo Mwenyeji Apone kwani zara yake mkoani hapa inazidisha
matumaini kwa wakazi wa Mkoa wa Tabora na jirani zake ya kuendelea
kufunguka milango au fursa mbalimbali za uchumi baada ya kuzindua miradi
mbalimbali ya miundo mbinu.
Bw. Mwanri alitoa wito kwa niaba ya wananchi wa Tabora kuwakaribisha wananchi kujotokeza kwa wingi kumlaki na kumsikiliza Rais Magufuli
0 comments:
Post a Comment