Mbunge
wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akisalimiana
na wachezaji wa Kata ya Nkiniziwa wakati wa ufunguzi rasmi wa michuano
ya Kigwangalla Cup 2017, iliyofanyika kwenye viwanja vya shule ya
Msingizi Nkiniziwa, timu hizo zilitoka droo ya bao 1-1.
Mbunge
wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akisalimiana
na timu ya Kata ya Mzibaziba wakati wa ufunguzi rasmi wa michuano ya
Kigwangalla Cup 2017, iliyofanyika kwenye viwanja vya shule ya Msingizi
Nkiniziwa, timu hizo zilitoka droo ya bao 1-1.
Mbunge
wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia)
akizungumza na wachezaji wa timu za Kata za Nkiniziwa na Mzibaziba
wakati wa ufunguzi rasmi wa michuano ya Kigwangalla Cup 2017,
iliyofanyika kwenye viwanja vya shule ya Msingizi Nkiniziwa, timu hizo
zilitoka droo ya bao
Mashindano
ya mpira wa miguu kwa timu za Kata zilizo ndani ya Jimbo la Nzega
Vijijini maalufu kama ‘Kigwangalla Cup’ yamezinduliwa rasmi jioni ya
Julai 27, 2017 huku miamba 20 ikitarajiwa kuumana kumpata bingwa wa
Jimbo hilo kwa mwaka huu.
Awali
akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye
pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla aliwataka wachezaji wote wanaoshiriki
michuano hiyo kuwa na nidhamu iliwaitumie michuano hiyo kama kipimo cha
wao cha kuonesha vipaji vyao ili waonekane ngazi za juu.
“Mpambane
kweli kweli. Kila mmoja wenu aoneshe uwezo wake wa kusakata kabumbu.
Pia muzingatie nidhamu ya hali ya juu kwani michezo inaleta umoja na
amani, inaimalisha afya ya miili yetu” alieleza Dk. Kigwangalla wakati
akuzungumza na wachezaji katika ufunguzi wa michuano hiyo.
Dk.
Kigwangalla pia alipata wasaha wa kukagua timu zilizofungua rasmi
michuano hiyo kati ya Mizibaziba dhidi ya Nkiniziwa ambazo hadi kipyenga
cha mwisho ziliweza kutoka droo ya bao 1-1.
Dk.
Kigwangalla alieleza kuwa, jumla ya Kata 19 za jimbo lake hilo zimeweza
kutoa timu ilikushiriki michuano hiyo huku timu maalum ikiingizwa
ambayo itajumuisha Madiwani wote kutoka Kata hizo ili kufanya jumla ya
timu 20.
Dk.
Kigwangalla alizitaja baadhi ya Kata zinazochuana kwenye michuano hiyo
ni pamoja na Kata ya Puge, Ndala, Nata, Sanzu,Lusu, Milambo Itobo,
Magengati,Budushi, Nkiniziwa, Mbagwa, Mizibaziba, Utwigu, Muhugi.
Kata zingine ni Kata za Mwantundu, Wela, Mwasala, Tongi, Ugembe na Mwakanshanhala.
Awali
kabla ya kuanza rasmi kwa mchezo wa ufunguzi, Madiwani wa Kata zote
waliweza kukabidhiwa baadhi ya vifaa kwa timu zao sambamba na hilo
wananchi waliweza kufurahia michezo mbalimbali ikiwemo ile ya jadi hasa
mchezo wa asili wa bao la Kinyamwezi, kucheza drafti, kukimbiza kuku,
michezo ya mbio kwa Wazee huku mchezo wa mbio kwa watu wenye vitambi
ukitia fola kwenye ufunguzi huo, uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya
Msingi Nkiniziwa iliyopo kwenye Kata hiyo ya Nkiniziwa.
0 comments:
Post a Comment