Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na. Paschal Dotto-MAELEZO
Serikali
ya Awamu ya Tano inaonyesha dhamira ya dhati ya kujenga Taifa lenye
uchumi wa viwanda. Ujenzi wa viwanda utapunguza ama kuondoa changamoto
ya ukosefu wa ajira hasa kwa vijana. Fursa za uwekezaji katika viwanda
ni jambo ambalo Mhe. Rais John Pombe Magufuli amekuwa akilisisitiza
katika hotuba zake.
Kwa
kuzingatia hilo, wajasiriamali na wawekezaji wameaanza kujitokeza
katika ujenzi na ufufuaji wa viwanda. Katika makala hii utamwona
mtanzania ambaye amebuniu teknolojia ya kutengeneza mkaa bila kuathiri
mazingira.
Mjasiramali
huyo ambaye ametumia fursa hiyo ni Bwana Leonard Gabriel Kushoka
ambaye ameanzisha kampuni ya kutengeneza na kuchakata nishati ya mkaa
kwa kutumia mashine maalumu katika kampuni yake ya Kuja na Kushoka Tools
Manufactured Group ambayo makao yake yako Tabora.
Hii
ni teknolojia ya pekee ambayo utapata nishati ya mkaa bila kuathiri
mazingira pia inatoa mwelekeo mzuri katika kuelekea uchumi wa taifa la
viwanda ambayo ni sera ya Serikali yetu ya Awamu ya Tano chini ya Dkt.
Magufuli , katika kutambua mchango wa wadau mbalimbali Serikali inaunga
mkono kwa yeyote mwenye fikra pana juu ya teknolojia yeyote anapaswa
kutoa wazo.
Kushoka
amesema katika upande wa mazingira kitu kikubwa kinachohitajika ni
kuyatunza kwa kuyaweka katika hali nzuri lakini pia kwa kupanda miti na
kuitumia ipasavyo katika kupata hewa safi.
Katika
mkutano wake na waandishi wa habari jijini Da es Salaam tarehe 12 Julai
2017 Kushoka alikuja na mashine ambayo kwa hakika ni mashine ya
kujivunia kwa Tanzania kuelekea uchumi wa viwanda. Katika mkutano huu
mashine hiyo ambayo kwa lugha ya kigeni inaitwa “Charcoal Ubiquity”
ambayo ina uhakika wa kuzalisha mkaa bila kuathiri mazingira ya binadamu
na watumiaji wa nishati hii muhimu ilitolewa ufafanuzi.
Kwa
mujibu wa takwimu za Wakala wa Misitu (TFS) Dar es Salaam inatumia
magunia 28000 ya nishati hiyo ambayo ni sawa na tani 1600 kwa siku
ambayo ni sawa na asilimia 50 kwa nchi nzima huku majiji ya Mwanza na
Arusha wakifuatia katika takwimu hizo. Kushoka anasema pia katika kupata
nishati hiyo kienyeji inatumia tani 12 za miti kwa tani 1 moja ya mkaa
kwa hiyo kwa takwimu hizo za Dar es Salaam zinaonyesha ni jinsi gani
uharibifu wa mazingira unatokea katika misitu asili ya nchi yetu.
Katika
matumizi sahihi ya teknolojia hii ya Kushoka Tools Manufactured Group
ni kujivunia kwa nchi yetu kuelekea kutimiza sera ya awamu ya tano
inayoelekea kuijenga Tanzania ya viwanda , mashine hii yenye kutumia
takataka za aina yeyote ikiwemo mabaki ya mazao isipokuwa plastiki
katika kuzalisha mkaa kwa matumizi ya nyumbani
Katika
teknolojia yake Bwana Kushoka alisema mashine hii ina uwezo wa
kuzalisha wastani kilo 160 kwa saa moja , pia inahitaji watu 7 katika
ufanyaji kazi wake ambao wanahitajika kwa kuiwezesha katika kuchakata
nishati hiyo ya mkaa, na ina uwezo wa kutoa magunia 20 kwa siku jambo
ambalo linarahisisha maisha na matumizi ya nishati hiyo majumbani.
Katika
ufumbuzi huu ambao pia utakuwa bora kwa kutoa ajira kwa vijana kwani
katika viwanda vidogo vidogo vitakvyoanzishwa vitakuwa na watumishi na
kusaidia kuondoa kero ya ajira kwa vijana
Bwana
Kushoka anasema kuwa malighafi zinazotumika katika mashine hiyo ni
takataka za aina yoyote isipokuwa vitu vya plastiki, kwa hiyo kwa
watumiaji wa mashine hii wanapaswa kujua kuwa plastiki siyo malighafi ya
mashine hii. Kwa takwimu za mazingira jiji la Dar es Salaam linazalisha
tani 5000 kwa siku kwa hiyo ni vyema teknolojia hii ikatolewa kwa elimu
kubwa ili kusaidia utunzaji wa mazingira.
Katika
matumizi ya mashine hii ni kitu ambacho ni muhimu zaidi katika kutumia
teknoljia hii, zaidi mashine hii ya kujivunia kwa nchini yetu inatumia
nishati ya mafuta ya diseli na umeme lakini sanasana inategemea na
maamuzi ya mtumiaji au mnunuzi wa mashine hii, ila kwa wale walioko
vijijini ambako hasa nishati ya umeme haipatikani kirahisi wanashauriwa
kupata mashine itumiayo diseli ili kuepusha usumbufu wa matumizi ya
teknolojia hii.
Akizungumzia
mabaki ya mazao kutoka mikoa ambayo huzalisha mazao mbalimbali ikiwemo
tumbaku, karanga, mpunga, mahindi, Kushoka alitaja baadhi ya mikoa hiyo
kuwa ni Tabora, Shinyanga, Mwanza na Rukwa. Maeneo hayo yanapswa kupata
teknolojia hiyo ikizingatiwa malighafi inapatikana kiurahisi na
kutumika katika kuchakata mkaa hatua ambayo inasaidia kutunza uoto wa
asili nchini.
Katika
matumizi ya mashine hii ni kitu ambacho ni muhimu zaidi katika kutumia
teknoljia hii, zaidi mashine hii ya kujivunia kwa nchini yetu inatumia
nishati ya mafuta ya diseli na umeme lakini sanasana inategemea na
maamuzi ya mtumiaji au mnunuzi wa mashine hii, ila kwa wale walioko
vijijini ambako hasa nishati ya umeme haipatikani kirahisi wanashauriwa
kupata mashine itumiayo diseli ili kuepusha usumbufu wa matumizi ya
teknolojia hii.
Kwa
Dar nes Salaam tayari kuna vituo vinne ambayo elimu kuhusu teknolojia
hii ishatolewa vituo kama Pugu, Tandika, Tegete pamoja na Mbezi Kimara
kwa hiyo kwa wakazi wa jiji la dar es salaam wanatakiwa kutembelea vituo
hivyo kwa elimu na kupata mashine hiyo yenye teknoljia ya kisasa
Kwa
watanzania wote tunatakiwa kuunga mkono jitihada hizi kubwa zinazo
fanywa na kuja na kushoka tools manufactures group, kwa kununua mashine
kwa matumizi kuchakata mkaa na kutunza mazingira kwa usafi wa nchi yetu
kwa maendeleo ya taifa, kupata mashine hii ya kujivunia katka mapinduzi
ya viwanda inategemea na mahitaji ya mnunuzi kwani mashine hii inauzwa
kuanzia shilingi milioni 3 mpaka milioni 15 kutokana na maamuzi lakini
bila kusahau matumizi ya mtumiaji katika teknolojia hii ya kisasa.
Taifa
letu, serikali ni yetu, mistu ni yetu tunatakiwa kutumia mazingira
vizuri kwa kupanda na kutunza mistu yetu ,nunua mashine ya kuchakata
mkaa ili kuepusha ukataji miti ovyo na kuharibu mazingira.
1 comments:
Ndugu yangu Hongera saaana. Je, Kituo cha Tandika kipo sehemu gani,.
Naomba namba ya simu ya wahusika... namaba yangu ni 0625962047
Post a Comment