WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema tumbaku ni siasa na tumbaku ni
uchumi na ameitaka Bodi ya Tumbaku itakayoundwa ijipange kumlinda
mkulima. Waziri Mkuu alitoa agizo hilo juzi wakati akizungumza na
watumishi wa idara za kilimo na ushirika na viongozi wa wilaya za mkoa
huo kwenye kikao alichokiitisha ili awape maagizo maalumu.
Kikao hicho kilihudhuriwa pia na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo,
Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia kilimo, Mathew Mtigumwe na baadhi ya
wakurugenzi kutoka wizara hiyo.
Alisema wajumbe wa bodi hiyo walishatajwa lakini kwa sasa hivi
wanasubiri uteuzi wa Mwenyekiti wa bodi hiyo. Hata hivyo, Waziri
alimweleuk32 Katibu Mkuu wa Kilimo awaite wajumbe wa bodi hiyo wakutane
na kumchagua Makamu Mwenyekiti wa muda ili waanze kazi ya kukutana na
WETCU zao.
“Kwa sababu bodi ni ya nchi nzima, ni vema wakakutana na WETCU zao na
AMCOS zao ili waanze kukusanya taarifa ya tumbaku kutoka Chunya,
Namtumbo, Serengeti na mahali mengine ili wapeleke message hii ya msimu
ujao,” alisema Waziri Mkuu.
Alisema ili kuongeza ufanisi kwenye zao hilo, itabidi baadhi ya
majukumu ya bodi yapunguzwe ikiwemo kazi ya utoaji vibali vya
kusafirisha na kununua tumbaku. “Hivi kama kibali cha kuuza tumbaku ya
Namtumbo kinatolewa na Bodi ambayo makao makuu yake yako Tabora, sasa
utawezaje kufuatilia kutoka Tabora? Kwanini kazi hiyo isifanywe na chama
kikuu cha ushirika kilichopo huko?” alihoji Waziri Mkuu.
Alionya kwamba endapo bodi itaachiwa iingie kila mahali, haitaweza
kulaumiwa pindi jambo likiharibika. “Ninyi kazi yenu kubwa iwe ni
usimamizi kuanzia kwenye WETCU na AMCOS zake. Simamieni masoko,
hakikisheni wanaokuja kununua wako tayari kufuata mfumo uliowekwa na
serikali,” alisema.
Alisema bodi ijayo inalo jukumu pia la kushirikiana na vyuo vya
utafiti ili kuhakikisha tafiti zinafanyika na kupata mbegu bora zenye
kustahimili magonjwa na hali ya hewa. Akizungumzia kuhusu upangaji wa
madaraja kwenye zao la tumbaku, Waziri Mkuu alisema kuna hatua
imefanyika kwani hivi sasa madaraja yamepunguzwa kutoka zaidi ya 100
yaliyokuwepo na kufikia 39. Hata hivyo, alisema wingi wa madaraja bado
ni changamoto kwenye upangaji wa bei.
“Bodi na wizara lazima mzungumze na makampuni ya ununuzi na
mkubaliane mfumo gani utatumika kuhusu madaraja ya tumbaku. Kazi yetu
kubwa na kumlinda mkulima. “Wenzenu wa korosho walikuwa na madaraja
mengi lakini sasa yamebakia mawili, grade 1 na grade 2 na bei ya kila
daraja inajulikana kwa hiyo si rahisi kumuibia mkulima,” alisisitiza
Naye Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tabora, Hassan Wakasuvi akitoa
shukrani kwa Waziri Mkuu kwa ziara yake, alisema wameyapokea maelekezo
hayo na hawatasita kuwasukuma watendaji wanaochelewa kutimiza wajibu
wao.
“Miaka miwili iliyopita, tumbaku ilikuwa zao linaloongoza kwa
kuingiza fedha za kigeni hapa nchini. Lakini hivi sasa tumeshuka, na
tumeiacha korosho ndiyo inaongoza, tumedhamiria kurudi kwenye nafasi
yetu, na hatutasita kuwaweka pembeni watendaji wa serikali
watakaotuchelewesha kufikia azma yetu hiyo,” alieleza.
Waziri Mkuu amemaliza ziara yake ya siku nne na ameahidi kurudi
kumalizia wilaya za Nzega, Igunga na Tabora Manispaa ambazo
hakuzitembelea.
CHANZO HABARI LEO
0 comments:
Post a Comment