Home » » RC TABORA ATOA MWEZI MMOJA KWA MWEKEZAJI WA KIWANDA CHA MAZIWA TABORA KUHAKIKISHA ANAFANYA UZALISHAJI

RC TABORA ATOA MWEZI MMOJA KWA MWEKEZAJI WA KIWANDA CHA MAZIWA TABORA KUHAKIKISHA ANAFANYA UZALISHAJI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


Na Tiganya Vincent, TABORA.

Mkuu wa Mkoa Tabora Bw. Aggrey Mwanri ametoa mwezi mmoja kwa mmiliki wa kiwanda cha Maziwa cha Tabora kuhakikisha anarekebisha kasoro zilizosababisha kufungwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa mwaka 2016 la sivyo Serikali itakichukua na kumpa mtu mwingine ili akiendeshe.

Bw. Mwanri alitoa agizo hilo jana mjini Tabora baada ya kutembelea Kiwanda ili kujionea mazingira yaliyosababisha kisimamishwe. Alisema kuwa mara baada ya kipindi cha mwezi kukamilika na kama Mmiliki wake atakuwa ajarekebisha mapungufu aliyoelekezwa na TFDA ayafanyie kazi itabidi apelike mapendekezo katika Wizara inayohusika na Viwanda ili kikabidhiwe kwa mwekezaji mwingine.

Mkuu wa Mkoa huyo aliongeza sanjari na kumwagiza alerebishe kasoro pia alimtaka apelike Mkataba wa Ununuzi wa Kiwanda hicho ili kuona kama anazingatia masharti aliyopewa wakati akikinua mwaka 1998. Kwa upande wa Meneja wa Kanda ya Magharibi wa TFDA Dkt.Edgar Mahundi alisema kuwa walipofanya ukaguzi katika kiwanda hicho walikuta maziwa yakizalishwa katika mazingira ambayo ni hatari kwa afya ya watumiaji.

Alisema kuwa wakikuta mrundikano wa maji machafu kuzunguka Kiwanda na kumwangiza ajenge mtaro wa kuyaondoa lakini hadi hivi sasa ameshindwa kuujenga. Dkt. Mahundi aliongeza kuwa jambo jingine aliagizwa kuhakikisha kuwa anakuwa na maabara na wataalam wa kutoka katika Kiwanda chake lakini ameshindwa kutekeleza maagizo hayo.

Alisema kuwa TFDA iko tayari kumfungulia kama atatekeleza maagizo waliompa ambayo yanalenga kulinda afya za watumiaji wa bidhaa zake.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited : |
Copyright © 2012. Tabora Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za mikoa