Na Tiganya Vincent
RS-TABORA
20 SEPTEMBA 2017
SERIKALI
ya Mkoa wa Tabora imeagiza kukamatwa na kuwekwa ndani kwa watumishi
wanne wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga na Mzabuni Muhoro Traders kwa
tuhuma za udanganyigu wa ununuzi wa vifaa tiba vyenye thamani ya
shilingi milioni 23.2.
Agizo hilo limetolewa leo mjini Igunga na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri katika taarifa yake kwa vyombo vya habari.
Amesema kuwa kwa nyakati tofauti za kuanzia Januari na
Machi mwaka huu watumishi walikula njama na kujipatia fedha kwa njia ya
udanganyifu jumla ya shilingi milioni 23,202.500.00 mali ya Halmashauri
ya Wilaya ya Igunga.
Mwanri
anaongeza kuwa watumishi hao waliagiza vifaa hivyo kutoka kwa Mzabuni
Muhoro Traders wa Igunga vifaa , lakini havikuwahi kupokelewa na
Halmashauri ya Igunga lakini kwenye vitabu vya Afisa Ugavi na yule wa
Bohari walikiri kupokea katika vitabu vyao.
“Naagiza
watumishi hao wanne wasimamishwe kazi na wakamatwe wao na Mzabuni
Muhoro Traders kisha wawekwe ndani kwa ajili ya kufikishwa Mahakamani ili wajibu tuhuma zinazowakabili” anasema Mkuu huyo wa Mkoa.
Anasema
kuwa katika hati namba ya malipo namba 2071-1457 watuhumiwa walichukua
shilingi 9,250,000/-, hati namba 2017-1457 walijipatia shilingi
6,850,000/- na hati ya malipo namba 2017-1453 shilingi 7,102,500/- na
kusababishia Halmashauri hasara hiyo.
Mwanri
amewataja walikamatwa ni pamoja na aliyewahi kwa Kaimu Mganga Mkuu wa
Wilaya ya Igunga Gidfrey Mgongo, Afisa Ugavi Mohamed Mtao, aliyekuwa
Mhasibu wa Idara ya Afya sasa yuko TARURA Richard Byelembo, Boharia wa
Idara ya Afya Jones Lotto.
Aidha
Mkuu huyo wa Mkoa ameagiza pia Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Igunga wa
sasa Dkt. Bonaventura Kalumete ili kupisha uchunguzi wa tuhuma hizo.
Katika
hatua nyingine Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mwanri amewaagiza kushughulikia
tatizo la ukosefu wa dawa katika Zahanati kwa sababu tayari Halmashauri
hiyo imepokea miliomi 550 kwa ajili ya kuboresha huduma za afya.
Mwisho
0 comments:
Post a Comment