Na Tiganya Vincent
RS-Tabora
23 Septemba 2017
Kanisa
Katoliki Jimbo Kuu la Tabora limeitaka jamii pamoja katika kuungana
katika kuwalinda ,kuwaheshimu na kusihi nao watu wenye ulemavu wa ngozi
ili nao waweze kutembea kifua mbele katika nchi hii kama walivyo watu
wengine.
Kauli
hiyo ilitolewa jana mjini hapa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki
mkoani Tabora Mhashamu Paulo Luzoka wakati wa ufungaji wa mafunzo ya
siku mbili juu ya kuwahudumia watoto wenye ulemavu wa ngozi.
Alisema
kuwa ni wajibu wa jamii nzima bila kujali tofauti zake za kiimani
kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha kuwa haki ya kuishi watu
wenye ulemavu wa ngozi inalindwa na kuwafanya waishi kwa amani na
furaha.
Mhashamu
Luzoka alisisitiza kuwa ni vema jamii ikaweka nguvu katika kuelimisha
jamii kuachana na vitendo vya kikatili dhidi ya watu wenye ulemavu kwa
imani za kishirikina ambavyo vinawafanya watu hao wasiishi kama watoto
yatima.
Alisema
kuwa hatua hiyo itasaidia kuwafanya waishi bila hofu na hivyo kuwa huru
katika kushiriki shughuli mbalimbali za maendeleo katika maeneo yoyote
ya nchi hii.
“Tusingependa
kuona kuwa dawa ya watu hao ikendelea kumwagika kwa sababu ya ulemavu
wao…jifikie wewe ungekuwa katika hali hiyo nawe ukatendewa kama
wanavyofanyiwa watu hao ungejisikiaje ? kama wewe unapenda kutendewa
jambo jema basi mtende na wewe albino jambo jema” alisema Askofu huyo wa
Jimbo Kuu la Tabora.
Alisisitiza
kuwa kama jamii itaungana na kuishi kwa amani basi hakutakuwepo na
mauaji ya watu wenye ulemavu na wazee kwa sababu ya umri wao kuwa mkubwa
na macho kubadilika.
Awali
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri alilishukuru Kanisa kwa mpango wa
kukabiliana na unyanyapa kwa watoto wenye ulemavu katika jamii wakiwemo
albino.
Alisema
kuwa Serikali ya Mkoa wa Tabora itasimama imara kukabiliana na tatizo
hilo ikiwemo kuwakata watu wote wenye imani za kishirikina ambayo
wamekuwa wakimwaga damu za watu wenye ulemavu wa ngozi kwa mawazo ya
kijinga kuwa watapata utajiri.
0 comments:
Post a Comment