.................................
Na Victor Makinda, Igunga
Zaidi ya wafugaji 3000 na wadau wengine wa sekta hiyo hiyo, kutoka maeneo mbali mbali nchini, wamekutana wilayani Igunga mkoani Tabora kwa ajili ya kufanya Kongamano kubwa la kujadili mafanikio na changamoto zinazoikabili sekta hiyo.
Hayo yameelezwa leo mjini Igunga na Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Wafugaji
Tanzania (CCWT) Ally Manonga (pichani)
Manonga amesema kuwa serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia
Suluhu Hassan, imetatua matatizo mengi yaliyokuwa yakiikabili sekta ya ufugaji
nchini, zipo changamoto chache zinazoikabili ambazo bado zinaikabili sekta
hivyo hivyo kongamano hilo litajadili na kupendekeza utatuzi wa changamoto
hizo.
"Matatizo mengi ya wafugaji yametatuliwa, bado yapo machache ambayo
pia yanatakiwa kutupiwa jicho ili kuyapatia ufumbuzi wa kudumu". Amesema.
Manonga amesema kuwa katika kongamano hilo watajadili mafanikio, changamoto na
namna ya kutatua changamoto zilizosalia.