Na Lucas Macha
Jeshi la Polisi mkoani Tabora limekatamata mabomu manne tofauti yaliyolenga kutumika katika tukio la uhalifu katika moja ya minada inayofanyika mkoani hapa.
Kamanda wa Polisi mkoani Tabora, Anthony Rutta, alisema jana kuwa mabomu hayo yanasadikiwa kuangizwa kutoka nchi jirani kwa lengo la kufanyia uhalifu mkoani humu.
Kamanda Rutta, alisema mabomu hayo yalikamatwa Agosti 16, mwaka huu katiki kata ya Ilolangulu wilaya ya Uyui mkoani humu.
Alisema kukamatwa kwa mabomu hayo kulitokana na raia wema kutoa taarifa kwa polisi kwamba katika nyumba ya mkazi wa kijiji hicho, Msindi Kasaki, kumehifadhiwa silaha hizo.
Kamanda Rutta alifafanua kwua baada ya kupata taarifa hizo, polisi walikwenda eneo la tukio na kumkuta mtuhumiwa.
Alisema baada ya kuhojiwa, mtuhumiwa huyo alikiri kuwa na mabomu hayo aliyokuwa ameyafukia nyuma ya nyumba yake yakiwa kwenye mfuko wa kiroba na ndani yake yamefungwa kwenye mfuko wa rambo.
Alisema utafiti uliofanywa na polisi umebaini kwamba mabomu hayo yalikuwa yamekusudiwa kwenda kufanya uhalifu kwenye moja ya minada ya wafanyabiashara ili kuwapora mali zao.
Kamanda Rutta alisema mabomu hayo yanasadikiwa kuingizwa nchini kutoka nchi jirani.
Aliwataka raia wema kuendelea kutoa taarifa kwa polisi kwa matukio yoyote wanayoyatilia shaka ili watuhumiwa wakamatwe.

Wakati huo huo, polisi mkoani Tabora wamekamata bunduki moja aina ya gombore linayotumia risasi za shotgun na risasi sita.
Pia wamefanikiwa kukamata maganda matatu ya shotgun na lita 70 za pombe haramu aina ya gongo pamoja na mitambo ya kutengezea pombe hiyo.
Hali kadhalika, katika msako huo, polisi wamekamata pikipiki 40 kwa kukiuka sheria za usalama barabarani.

Chanzo: Nipashe
0 comments:
Post a Comment