Home » » CHADEMA IGUNGA YAITAMBIA CCM

CHADEMA IGUNGA YAITAMBIA CCM

na Hastin Liumba, Tabora
MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wilaya ya Igunga, Hamis Majimoto, amesema chama hicho hakina wasiwasi na CCM muda wa uchaguzi utakapowadia jimboni humo.
Majimoto alitoa kauli hiyo alipozungumza na Tanzania Daima wilayani Igunga hivi karibuni na kusema kuwa ni dhahiri CCM ilipoka ushindi wao, lakini mkono wa sheria kupitia Mahakama Kuu Kanda ya Tabora, umefanya kazi yake bila ya upendeleo.
“Hoja zetu zote zilikuwa za ukweli na mashahidi wetu waliotoka maeneo mbalimbali tena kwa fedha zao, ili waje kutoa ushahidi na Mungu ametusikia kilio chetu,” alisema.
Aliipongeza kauli ya Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, kuwa CCM iheshimu maamuzi ya Mahakama Kuu.
“Haki ya mnyonge siku zote huwa haipotei, bali inacheleweshwa na sasa CCM tumewabwaga mahakamani,” alisema.
Alisema wao kama CHADEMA wilaya, wako tayari kwa uchaguzi na wana uhakika wa asilimia 100 kuwagaragaza CCM hata wakitoka usingizini.
“Tuko tayari kwa uchaguzi, iwe mdogo ama wa mwaka 2015…..ni lazima CCM ichezee kichapo tu, tumejipanga vema na hata wao wanajua tutawachapa,” alisema.
Chanzo: Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited : |
Copyright © 2012. Tabora Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za mikoa