Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk.Willibrod Slaa
Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk.Willibrod Slaa, akizunguma na
wananchi wa kijiji cha Tula jimbo la Igalula wakati wa ziara yake ya
wiki tatu ya kuimarisha chama katika mikoa ya Tabora, Kigoma na Singida,
alisema kadi hiyo ikiuzwa kwa kiwango hicho zitamsaidia kupata fedha za
kuanzishia mradi wa biashara.
“CCM wamewanyima ajira kwa hiyo mtu akija anataka kununua kadi ya
Chadema ruksa kumuuzia lakini msiuze chini ya Sh. 100,000 ili mpate
fedha za kuanzishia biashara, mkiuza kwa Sh.1500 haitawalipa,” alisema.
Alisema wakati wa uchaguzi mkuu wa 2010, serikali ya CCM ilitangaza
ajira 100,000 kwa vijana, lakini hadi sasa utekelezaji wake haupo na
katika hali ya kushangaza ajira hizo zimejumuishwa hata za wabeba
mikokoteni.
Katibu Mkuu katika baadhi ya majimbo ya mkoa wa Tabora alitoa ofa
kwa kuwanunulia kadi wanachama wapya zaidi ya 4,000 katika majimbo ya
mikoa ya Tabora na Singida.
Dk. Slaa akizungumzia amani alisema hivi sasa nchi inapitia katika
kipindi kigumu sana kutokana na matukio ya kutisha yanayotokea maeneo
mbalimbali hali inayotokana na wananchi kukata tamaa.
“Nchi ipo katika wakati mgumu wananchi wameanza kukosa uvumilivu
kwa manyanyaso ndiyo maana mara utasikia wananchi wamevamia kituo cha
polisi kwa lengo la kutaka kumtoa mtuhumiwa aliyekamatwa pengine kwa
kuonewa,” alisema.
Alisema Tanzania mtu asiyekuwa na pesa amekuwa kama kuwepo kwake
hapa duniani ni dhambi na mwenye pesa anaamua kufanya lolote kwa
asiyekuwa na pesa.
CHANZO:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment