Home » » Waathirika wa mafuruiko Manispaa Tabora wapewa msaada

Waathirika wa mafuruiko Manispaa Tabora wapewa msaada

KUFUATIA Mafuriko yaliyowapata wakazi wa Uzunguzi katika Manispaa ya Tabora na kuwapatia hasara ya mali na vyakula,Halmashauri ya Manispaa ya Tabora imetoa msaada wa chakula kwa waathirika hao wenye thamani ya Shilingi Milioni Moaja na laki mbili.

Akikabidhi msaada huo Meya wa Manispaa ya Tabora,Gullamhussein Dewji,amesema wameamua kutoa msaada huo mdogo ili kuwasaidia wananchi hao kwa vile wameathirika kwa vyakula vyao kuharibiwa na maji.

Mkuu wa wilaya ya Tabora,Suleiman Kumchaya ametaka msaada huo uwafikie walengwa na watafuatilia kuhakikisha walengwa kama wamepata msaada huo wa chakula

Kwa upande wao wakazi wa eneo hilo wameshukuru kwa msaada huo uliotolewa na Halmashauri ya Manispaa ya Tabora na kwamba utawatosha angalau kwa siku mbili au tatu.

Wakazi wa eneo hilo walikumbwa na mafuriko wakati wa sikuku za X.mass kufuatia mvua kubwa iliyonyesha siku ya tarehe Ishirini na Nne,Sikukuu ya Krismas na Tarehe Ishirini na Saba na kusababisha uharibifu mkubwa wa mali zao na vyakula.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited : |
Copyright © 2012. Tabora Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za mikoa