Home »
» 3 wafa kwa kula uyoga wa porini
3 wafa kwa kula uyoga wa porini
Watu
watatu wakazi wa Kijiji cha Igunguli, Kata ya Uyogo, Wilaya ya Urambo,
mkoani Tabora, wamefariki dunia baada ya kula chakula kinachodhaniwa
kuwa na sumu.
Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo, Dkt. Kheri Kagya,
alisema chakula hicho kililiwa na watu wanane ambacho ni ugali na mboga
ya uyoga uliochumwa porini ambao ndio unadhaniwa kuwa na sumu.
Waliofariki
ni watoto Kija Makoye (3) akiwa njiani kupelekwa Hospitali ya Wilaya
hiyo, Wande Mahinge (5) na Mahigi Tongele ambao walikufa wakati
wakipatiwa matibabu.
Dkt. Kagya alisema baadhi ya walionusurika
katika tukio hilo ni pamoja na mtoto Gimili Makoye (miezi kumi), Talekwa
Mahigi (3) na mpishi wa chakula hicho, Nyanzobe Mswahili (25).
"Tulishindwa
kuchukua sampuli ya chakula kinachohisiwa kuwa na sumu kwa sababu
kililiwa chote, hata aina ya uyoga tumeshindwa kuutambua kwa vile nao
ulichumwa wote.
"Mswahili alitueleza kuwa, uyoga aliochuma porini ulikuwa unafanana na waliowahi kula hivyo hatukuutambua," alisema.
Kamanda wa Polisi mkoani humo, Kamishna Msaidizi wa Polisi Peter Ouma, amethibitisha jeshi hilo kupokea taarifa za tukio hilo
Chanzo;Majira
0 comments:
Post a Comment