Igunga. Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema), Dk Willbroad Slaa, amehitimisha ziara yake wilayani
Igunga na kumtaka Rais Jakaya Kikwete kuwawajibisha Mkurugenzi wa
Usalama wa Taifa, Mkuu wa Jeshi la Polisi pamoja na Jeshi la Wananchi
Tanzania (JWTZ) kutokana na sakata la Operesheni Tokomeza Ujangili
(OTU).
Vile vile, amemuonya Mbunge wa Kigoma Kaskazini,
Zitto Kabwe kwa kusema kuwa anakabiliwa na tishio la kufukuzwa uanachana
kutokana na kuwepo na vikaratasi vinavyogawanywa kupinga uamuzi wa
Kamati Kuu ya Chadema.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika
katika Viwanja vya Barafu, Igunga, Dk Slaa alisema kwamba Rais Kikwete
anapaswa kuwawajibisha iwapo hawatafanya hivyo ili kujijengea heshima
katika kipindi cha miaka miwili ya utawala wake uliobakia.
Alisema katika taarifa ya Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira kuhusu Operesheni Tokomeza
Ujangili, iliyowasilishwa Bungeni, Serikali na vyombo vya dola
vimeumbuka kutokana na kubainika kuwa vilihusika katika kuwatesa raia,
kuwaua ikiwa ni pamoja na kupora mali zao, hivyo kwa vile watekelezaji
walikuwa ni idara ya usalama wa Taifa, Polisi na Jeshi la Wananchi bado
wakuu wake wanapaswa kujiuzulu kutokana na aibu hiyo.
“Kule Serengeti mkoani Mara walimkamata kijana
wetu, tena Diwani wa Chadema na kumlazimisha kukiri kuwa alikuwa
akimiliki bunduki na kuwinda tembo, alipokataa walimpiga shoti ya umeme,
wakamwekea waya wa baiskeli na kuusokota, lakini kule Babati
wamemkamata mama wakidai kuwa alikuwa akiua tembo na kumbaka kwa zamu,”
alieleza Dk Slaa.
Alisema kwamba mateso haya yanafanyika sasa na
vyombo vya dola baada ya kufanywa kwa muda mrefu na watendaji wa vijiji,
wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa, lakini licha ya kwamba njia ya
kuondoa kero hizo za manyanyaso kwa wananchi hazihitaji fedha, lakini
bado Serikali imekuwa ikishindwa kuchukua hatua.
Alisema watu wanabambikiwa kesi za mauaji kwa
makusudi, Serikali ipo ikiangalia pamoja na vyombo vya usalama wa Taifa,
hivyo kuwataka wakuu wake nao kufuata njia za mawaziri wanne kwa
kujiuzulu ili kulinda hadhi ya taasisi zao.
“Polisi walikamata vijana wetu wa Chadema wakati
walipokuwa wakitaka kutubambikia kesi ya ugaidi, waliwapeleka kule
Tabora waliwatesa na umeme mateso makali sana, waliwachanachana kwa visu
vya bunduki sehemu zao za siri na kuwawekea waya, mateso haya ni makali
na yamefanywa kwa vijana ambao wameoa juzi, bora hata wangefanya kwangu
mimi mwenye umri mkubwa,” alieleza kwa masikitiko.
Alipokuwa katika Wilaya ya Nzega, Dk Slaa,
alimuonya Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe kuwa anakabiliwa na
tishio la kufukuzwa uanachama kwa kile kinachoendelea kwa sasa ndani ya
chama.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika
Nzega Mjini alisema chama kimepokea taarifa za mpango wa kundi la watu
ambao wanasadikiwa kuwa wafuasi wa Zitto kupitisha karatasi na
kusainisha majina ya wanachama kwa lengo la kuandaa pingamizi dhidi ya
uamuzi wa chama jambo ambalo alisema litamponza
Chanzo;Mwnanchi
0 comments:
Post a Comment