WAENDESHA
Pikipiki maarufu kama Bodaboda Wilayani Tabora wamewalalamikia Askari wa Doria
wanaoendesha pikipiki kuwa wanawanyanyasa na kuwaomba Rushwa wakiwa kwenye
majukumu yao.
Wakizungumza
kwenye kikao cha wamiliki wa pikipiki na madereva Bodaboda,wamesema askari wa
Doria wanaotumia Pikipiki ni kero kubwa kwao na kutaka hatua za kinidhamu
zichukuliwe dhidi yao.
Wakijibu
malalamiko hayo,Mkuu wa Polisi Wilaya ya Tabora Samwel
Mwampashe na Msimamizi wa makosa ya usalama barabarani Mkaguzi Swalehe Digega
wamesema Jeshi la Polisi lipo kwa lengo la kusimamia Sheria na sio kupotosha
kwani wapo baadhi ya madereva sio waaminifu na kuwataka kutii sheria bila
shuruti
Naye
Mkuu wa wilaya ya Tabora,Bw.Suleiman Kumchaya amekubali maombi ya waendesha
Bodaboda hao kupata elimu kuhusu usalama barabarani ili kupunguza ajali na
kuwapunguzia kazi askari wa usalama barabarani.
Kwa
mujibu wa Afisa usalama barabarani wilaya ya Tabora,Swalehe Digega, madereva wa
bodaboda manispaa ya Tabora hawazingatii sheria za usalama barabarani
hivyo husababisha ajali kati ya tatu hadi tano
0 comments:
Post a Comment