WAKAZI wa Kijiji cha
Lumbe, Kata ya Ukumbisiganga, wilayani Kaliua mkoani Tabora, wamelalamikia
faini ya sh 180,000 wanayotozwa kwa kila ng’ombe anayeingia katika hifadhi ya
taifa na kusema faini hiyo haiwatendei haki.
Walitoa kauli hiyo
hivi karibuni mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Fatma Mwassa, aliyetaka kujua
kero zinazowakabili wafugaji wa kata hizo.
Akizungumza kwa niaba
ya wafugaji wenzake, Gunze Pamagi, alisema hivi karibuni baada ya ng’ombe wao
zaidi ya 5,000 kuingia kwa bahati mbaya katika hifadhi ya taifa, walikamatwa na
kila ng’ombe mmoja alitozwa sh 180,000, badala ya sh 30,000.
Walisema hatua hiyo
imewashangaza hata kufikia mahali wanahisi watu wa Maliasili hulazimisha
kutaifisha mifugo yao kwa nguvu kwa ajili ya kujipatia fedha kutoka kwa
wafugaji.
“Ni kweli mifugo yetu
ilikamatwa katika hifadi ya taifa na baada ya hapo sisi tuko tayari kulipia
faini hiyo lakini tunakatishwa tamaa na faini ya sh 180,000, hapa tunaona kama
tunaibiwa,” alisema Pamagi.
Akijibu malalamiko
hayo, Mwassa alisema licha ya kujionea hali hiyo, wafugaji wanapaswa kutambua
kuwa zoezi linaloendelea ni la kitaifa na si la mkoa.
Alisema atakachofanya
ni kumuomba waziri mwenye dhamana ili wafugaji waweze kulipa faini sitahiki.
Sina uamuzi mwingine
kwa sasa mpaka niwasiliane na waziri mwenye dhamana ili mlipe faini stahiki,
ila tambueni serikali inajua changamoto mnazokabiliana nazo,” alisema Mwassa.
Chanzo: Tanzania
Daima
0 comments:
Post a Comment