Na Hastin Liumba,Uyui
WAJUMBE ALAT TABORA WATEMBELEA MIRADI YA MILIONI 843.
WAJUMBE wa ALAT mkoa wa Tabora,wamepongeza na kuridhika na miradi ya
halmashauri ya wilaya ya Uyui kuwa inalingana na thamani ya fedha
zilizotumika.
Hatua hiyo ilikuja wakati walipokuwa kwenye ukaguzi wa miradi hiyo
ambapo walisema hali hiyo itarejesha imani kwa wananchi jinsi fedha za
maendeleo zinavyotumika.
Miradi iliyotembelewa ni mitano na ina thamani yajumla ya sh milioni
843,891,850.
Miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa daraja la Kalemela wenye thamani ya
sh milioni 72,743,000 na mradi wa ukarabati wa ghala la kuhifadhia
mazao mchanganyiko lenye thamani ya sh milioni 27.
Aidha miradi mingine ni ujenzi wa nyumba nane za watumishi wa
halmashauri hiyo wenye thamani ya sh milioni 567,816,640 na mradi wa
ujenzi wa ofisi ya kata ya Isikizya wenye thamani ya sh milioni
30,981,210.
Mradi mwingine ni ujenzi wa kituo cha polisi wilaya ya Uyui wenye
thamani ya sh milioni 145,351,000.
Aidha miradi hiyo iliyotembelewa baadhi ipo kwenye hatua za mwisho
huku mingine ikiwa imeshakamilika.
Katika hatua nyingine wajumbe wa ALAT mkoa wa Tabora wakichangia
kwenye kikao cha majumuisho walisema ipo haja ya kuomba kiwanja na
kujenga jengo la mkoa la kitegeuchumi.
Walisema suala hilo liangaliwe kwa kushirikisha watalaamu na maamuzi
yazingatie katiba ya ALAT inavyosema.
Home »
» WAJUMBE ALAT TABORA WATEMBELEA MIRADI YA MILIONI 843.
0 comments:
Post a Comment