Home » » POLISI WATUMIA NGUVU MABOMU YA MACHOZI KUTAWANYA MAANDAMANO YA WACHIMBAJI WADOGO KATIKA MACHIMBO YA MWASHINA WILAYANI NZEGA,KINGWANGALA AKAMATWA

POLISI WATUMIA NGUVU MABOMU YA MACHOZI KUTAWANYA MAANDAMANO YA WACHIMBAJI WADOGO KATIKA MACHIMBO YA MWASHINA WILAYANI NZEGA,KINGWANGALA AKAMATWA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.


Wachimbaji wakiandamana leo wilayani Nzega mkoani Tabora. 
Jeshi  la polisi wilayani Nzega mkoani Tabora limetumia nguvu kusambaratisha maandamano ya wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu yaliyolenga  kupinga kufungwa kwa machimbo yao ya Mwashina yaliyo jirani na mgodi wa Resolute Tanzania Limited wilayani Nzega.
Mara baada ya kukaribia katika eneo la machimbo ambako maandamano yalikuwa yanaelekea,kabla hata hawajafika eneo la machimbo,ghafla polisi waliibuka na kuanza kurusha mabomu hovyo na baadaye kumkata mbunge wa jimbo la Nzega Dkt Hamis Kigwangalla ambaye kabla ya kuanza kwa maandamano hayo alifanya mkutano wa hadhara katika kijiji cha Nzega ndogo ili kujua mstakabali wa wachimbaji hao ambao hivi karibuni waliziuiwa kuchumba na kamishana wa madini nchini Paul Masanja kwa kile kilichotajwa kuwa wamevamia eneo hilo

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited : |
Copyright © 2012. Tabora Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za mikoa