Hili
ndilo jiwe alilopigwa nalo mfanyabiashara wa vipuri vya pikipiki mjini Tabora marehemu Michael
Samson na kupasua eneo kubwa la
sehemu ya kichwa na kufariki papo hapo katika Bar ya Uhuru iliyopo mtaa
wa Madrasat Kata ya Kanyenye manispaa ya Tabora.
Kamanda
wa Polisi mkoa wa Tabora ACP SUZAN KAGANDA akizungumza na waandishi wa
habari ofisini kwake kuhusu mauaji ya mtu mmoja ambaye alikuwa ni
mfanyabiashara wa vipuri vya pikipiki mjini Tabora marehemu Michael
Samson ambaye aliuawa usiku baada ya kuvamiwa na watu wasiojulikana
ambapo walimpiga kwa jiwe kichwani lililosababisha kifo chake papo hapo.
Kwa mujibu wa mashuhuda
mmoja kati ya wauaji mara baada ya kuwaamuru walale chini wateja watano
waliokutwa kwenye Bar hiyo alichukua jiwe lililokuwa umbali wa hatua
kumi na kuja kumpiga nalo mara mbili kichwani kwa nguvu marehemu
Michael hali iliyosababisha kupasuka vibaya kichwa....Hata hivyo Polisi
hadi sasa wanawashikilia watu wawili kuhusiana na tukio hilo la kinyama.
CHANZO Kapipij blog
0 comments:
Post a Comment