Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
ZAHANATI zilizopo wilayani Igunga zinatarajiwa kufungwa umeme wa
jua ili kuwaepusha wananchi kuchangia mafuta ya taa wakati wanapohitaji
huduma nyakati za usiku katika zahanati hizo.
Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mwasungho, Kata ya Ngulu, juzi
katika ziara yake ya kuwahamasisha kujiunga na Mfuko wa huduma ya afya
ya jamii (CHF) Mkuu wa Wilaya hiyo, Elibariki Kingu, alisema
amewasiliana na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo
na kuahidi kulitekeleza suala hilo.
Alisema kuwa suala hilo litafanywa kwa haraka na kwamba kazi
iliyobaki sasa ni wataalamu wa masuala ya umeme vijijini (REA) kufanya
tathmini ya jumla ya namna ya kuweka umeme huo katika zahanati hizo.
Chanzo:Tanzania daima
0 comments:
Post a Comment