Home » » CCM yawaagiza Madiwani wake Igunga

CCM yawaagiza Madiwani wake Igunga

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

CHAMA cha Mapinduzi wilayani Igunga  kimewaagiza Madiwani wake  kuhakikisha wanasimamia kwa makini miradi yote ya maendeleo inayopelekwa na Serikali kwenye Kata zao.

Agizo hilo limetolewa na Mwenyekiti wa Chama hicho Wilaya ya Igunga, Bw. Costa Olomi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Mwisi uliohusu utoaji wa cheti bora cha ushindi kwa kata hiyo kwa kuongoza kiwilaya kwa kuingiza wanachama zaidi ya Mia tatu mwaka jana ikiwa ni pamoja na kusimamia vizuri ulipaji wa ada za wanachama wa Chama hicho.

Amesema endapo ,kila Diwani atasimamia vizuri  miradi iliyopo kwenye Kata yake ,kutaondoa manung'uniko toka kwa wananchi na kuendelea
kukiamini Chama hicho pamoja na Serikali iliyopo madarakani.

Ameonya kuwa Diwani  atakayeshindwa kusimamia vizuri fedha zinazotolewa na Serikali pamoja na michango inayochangwa na wananchi
kwa shughuli za maendeleo, Chama cha Mapinduzi hakitakuwa tayari kumvumilia kwa kuwa atakuwa ameshindwea kuwatumikia
wananchi waliomchagua.

Olomi ameongeza kuwa, kitendo cha Madiwani kutotambua matatizo ya wananchi kinaweza kuwasababishia kushindwa kuaminiwa tena
na wananchi wanaowaongoza.
 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited : |
Copyright © 2012. Tabora Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za mikoa