Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
ZAIDI
ya Wachimbaji wadogo 7000 katika mgodi mdogo wa dhahabu wa Mwanshina wilayani
Nzega mkoani Tabora wamepoteza ajira zao walizo jiajiri wenyewe baada ya ofisi
za madini kutoa masaa 48 kuondoka eneo hilo.
Kamishina
wa Madini Nchini Paul Masanja akizungumza na mwanachi amesema kuwa wachimbaji
hao wamevamia eneo la mwekezani Resolute ambapo hadi sasa bado lina milikiwa
kiharali na mgodi huo.
Amesema
kuwa kitendo cha kuvamie eneo hilo wachimbaji wadogo ni kuvunja sheria za
madini na kuongeza kuwa watu hao wanapaswa kuondoka ndani ya masaa
48 kuanzia sasa ili eneo hilo libaki wazi.
Wakizungumza
kwa nyakati mbalimbali baadhi ya wachimbaji katika mgodi huo wamesema kuwa
wamesikitishwa na kauli hiyo ya masaa 48 kuondoka eneo hilo huku wengine wakiwa
hawana pesa.
Juma
Ramadhani mkazi wa kahama amesema kuwa kitendo cha serikali kuwafukuza
wachimbaji wadogo nikuongeza waharifu ikiwa ni majambazi,vibaka pamoja na
wanawake kujiuza miili yao kutokana na ugumu wa maisha.
Alisema
kuwa serikali inapaswa kuwa makini katika maamuzi hayo ili wananchi wake waweze
kunufaika na rasilimali zao tofauti na kuwa wakimbizi ndani ya nchi yao kama
jinsi inavyo endelea hivi sasa.
0 comments:
Post a Comment