Na Hastin Liumba,Kaliua KATIBU wa Chama cha mapinduzi (CCM) kata ya Usinge wilaya ya Kaliua mkoani Tabora Hassan Salumu Ntama ana kesi kujibu katika mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Tabora baada ya kubainika ni mhamiaji haramu mwenye asili ya nchi ya Burundi. Katika cheti chake cha kuzaliwa kilikutwa na jina la Hassan Salumu Ntala,wakati jina lake halisi ni Fredrick Ntala. Kada huyo wa CCM amefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi kwa kesi ya jinai namba 221/2014. Katibu huyo wa CCM kata ya Usinge amefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi wa Tabora Bahati Chitepo kwa makosa ya kuishi nchini kinyume cha sheria namba S kifungu kidogo cha sheria 31 (i) (i) (2) kifungu cha sheria za Uhamiaji kifungu cha 54 ya mwaka 2002. Aidha kosa jingine ni kutoa taarifa za uwongo kwa afisa uhamiaji kifungu kidogo cha C/S 31 (i) (a) , (2) na kutumia cheti cha bandia cha kuzaliwa kinyume cha kifungu cha sheria namba C/S 31(i) (e) 2. Aidha Hassan Salumu Ntama alifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza mnamo mwezi machi 4 mwaka, 2014 ambapo upande wa mashitaka uliwasilisha ushahidi wake kwa kuita mashahidi wawili. Mashahidi wawili wa upande wa mashitaka walitoa ushahidi wao ni Konstebo wa uhamiaji Marinta Morumba wilaya ya Urambo na katibu tawala wa wilaya ya Urambo Pachael Byemela ili kuthibitisha makosa husika. Hata hivyo kutokana na ushahidi wao mahakama imejiridhisha kutokana na ushahidi wa upande wa mashitaka na kwa kuthibitisha kuwa katibu wa CCM kata ya Usinge wilaya ya Kaliua Hassan Salumu Ntama ni mhamiaji haramu toka nchini Burundi. Aidha chini ya mwanasheria wa Uhamiaji mkoa wa Tabora Charles Kasambula kada huyo wa CCM amepatina na hatia na anakabiliwa na kosa la jinai itaanza kwa mshitakiwa kuanza kujitete mwezi April 6 2014. Mapema mwaka mwaka jana mwishoni kufuatia zoezi la Operesheni Kimbunga likiendelea kuliripotiwa kuwa karibu uongozi wote wa kata ya Kaliua wa chama cha mapinduzi ni wahamiaji haramu. Taarifa hizo zilikuja kufuatia mkuu wa mkoa wa Tabora Fatma Mwassa kufanya mkutano wa hadhara kata ya Usinge wilaya ya Kaliua na kuomba wananchi kufichua wahamiaji haramu,majambazi na majangiri wanaoendesha vitendo viovu. Hatua hiyo inaonyesha kuzaa matunda baada ya kile alichotaka mkuu wa mkoa wa Tabora kutaka wahusiska kufichuliwa hadharani ili sheria ichukue mkondo wake.
Home »
» KADA CCM KATA YA USINGE AFIKISHWA MAHAKAMANI KUJIBU SHITAKA LA KUISHI NCHINI AKIWA RAIA WA BURUNDI.
KADA CCM KATA YA USINGE AFIKISHWA MAHAKAMANI KUJIBU SHITAKA LA KUISHI NCHINI AKIWA RAIA WA BURUNDI.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment