Na Hastin Liumba,Igunga
SERIKALI wilayani Igunga Mkoani Tabora imewataka wakulima wilayani
humo kutolipiza kisasi cha mauaji kwa wafugaji wa waishio wilayani
Kishapu mkoani Shinyanga ili vyombo vya Dola vifanye kazi yake.
Mkuu wa wilaya ya Igunga Elibarik Kingu alisema hayo katika mahojiano
na waandishi baada ya kutokea mauaji ya wakulima wanne kuuawa na
wafugaji wa wilaya ya Kishapu kutokana na wafugaji hao kudai eneo
wanalolima wakulima ni eneo lao.
Kingu aliwataka wafugaji hao wawe na uvumilivu kwa kipindi hiki kigumu
kwao na kuongeza serikali itachukua hatua kali za kisheria
ilikuhakikisha wale wote walio husika na mauaji ya watu hao
wanafikishwa mahakamani.
''Msilipize kisasi sisi kama serikali tupo makini tutahakikisha wale
wote waliofanya hivyo wanafikishwa mahakamani ili haki itendeke........
kuweni wavumili tu''alisema Kingu.
Kingu aliwapongeza wakulima hao kwa kutokujibizana na wafugaji hao na
badala yake waliondoka eneo la tukio hadi kukimbilia maeneo ya
wananchi ambako waliweza kupata hifadhi ya wanajamii husika.
Alisema kitendo cha kufanya malipizano nikuongeza maafa ambayo
yanaweza kuzuilika kwa mazungumzo na kuwataka wakulima hao kuendelea
na shuguli zao huku serikali ikiendelea kutafuta suruhu ya mgogoro
huo.
Kingu alisema kiburi cha wafugaji cha kufanya vurugu kina tokana na
jeuri ya kuhonga pesa baadhi ya maofisa wa vijiji na kata ambao sio
waaminifu kwa utendajikazi katika maeneo yao na kuongeza kuwa
serikali itafanya uchunguzi wa kina.
Mkuu wa mkoa wa Tabora Fatma Mwassa aliwahakikishia wa kulima hao
amani na ulinzi katika eneo hilo la shamba na kuongeza serikali
itahakikisha wote walio husika wanafikishwa mahakamani.
Mwassa alisema kuwa serikali inalaani vikali kitendo hicho cha
wafugaji cha kuwa aua wakulima wanne huku wengine 150 wakikosa
makazi,29 kujeruhiwa bila sababu za msingi katika maeneo yao.
Wakizungumza kwa nyakati mbalimbali baadhi ya wakulima wahanga wa
tukio hilo walisema wafugaji hao walivamia eneo hilo March 29 mwaka
huu majira saa kumi na mbili asubuhi walianza kuwashambulia.
Edward Lucas mkazi wa kata ya Isakamaliwa alilaani kitendo cha mkuu wa
wilaya ya kishapu Willison Nkhambaku kuwaachia wafugaji wa walio kuwa
wakituhumiwa kwa mauaji hadi kupeleka hadi sasa hakuna mtu anaye
shikiliwa na mauaji hayo ya watu wanne.
Home »
» SERIKALI YAWATAKA WAKULIMA KUTOLIPIZA KISASI KWA WAFUGAJI.
SERIKALI YAWATAKA WAKULIMA KUTOLIPIZA KISASI KWA WAFUGAJI.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment