Home » » DK KIGWANGALLAH WENZAKE 11 MAHAKAMANI

DK KIGWANGALLAH WENZAKE 11 MAHAKAMANI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Na Hastin Liumba,Nzega
 
 
MAHAKAMA ya Hakim mkazi wilaya ya Nzega Mkoani Tabora jana imemsomea
mashitaka matatu   mbunge wa jimbo la Nzega Dk Hamis Kigwangallah  na
watuhumiwa wenzeka 11 mbele ya hakim mkazi
 
MBUNGE wa jimbo la Nzega mkoani Tabora Dk Hamis Kigwangallah,wenake
11wamefikishwa mahakama ya hakimu mkazi wilaya na kusomewa mashitaka
matatu.
 
Mwendesha mashitaka wa Jeshi la polisi wilaya mkaguzi msaidizi Merito
Ukongoji akisoma mashata mbele ya watuhumiwa hao chini ya hakimu mkazi
wilaya ya Nzega Joseph Ngomello, alisema watuhumiwa wote 12
wanatuhumiwa kwa makosa matatu.
 
Akisoma makosa ya watuhumiwa hao alisema kosa la kwanza washitakiwa
wote 12 wanatuhumiwa kwa kosa la uhalibifu wa mali ya mgodi wa dhahabu
wa Resolute yenye thamani Milioni 15.9.
 
Kosa la pili kwa watuhumiwa hao wote 12 ni kufanya mkutano bila kibali
katika mji mdogo wa Nzega Ndogo, huku shitaka la tatu likiwa ni
kufanya maandamano bila kibali kitendo kinachoweza kusababisha
uvunjifu wa amani.
 
Aidha mwendesha mashitaka wa Jeshi la polisi Mellto Ukongoji  amesema
watuhumiwa wote 12 akiwemo mbunge wa jimbo hilo wapo nje kwa mdhamana
mpaka kesi itakapo tajwa tena, April 9 , mwaka huu.
 
Melito aliiambia mahakama hiyo kuwa watuhumiwa hao 12 walitenda
matukio hayo march 23 mwaka huu katika kijiji cha Nzega ndogo na
kukamatwa wakiwa pembezoni mwa mgodi mkubwa wa dhahabu wa Resolute
ikiwa na kufanya uhalibifu mkubwa.
 
Aliwataja watuhumiwa hao Dk Hamis Kigwangallah, Richard Mayunga ,Hamis
Charles, Bernard Bitus, Ibrahim Mrima, Fedrck Mbula, Peter Mandege,
Razalo Shimba, Maganga Seleli, Elikana Daud , Kankoba Sululi na
Luhende Shija.
 
Mwendesha mashitaka huyo aliiambia mahakama hiyo kuwa upelelezi bado
haujakamilika dhidi ya shauri hilo na kuongeza kuwa watuhumiwa wote 12
wapo nje kwa dhamana.
 
Hakim mkazi wa mahakama ya wilaya Joseph Ngomello aliahilisha kesi
hiyo huku shauri hilo litasomwa tena April 9 mwaka huu katika mahakama
hiyo ya hakim mkazi wilaya.
 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited : |
Copyright © 2012. Tabora Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za mikoa