Home » » VIJANA UNDENI VIKUNDI BILA KUJALI VYAMA VYA SIASA.

VIJANA UNDENI VIKUNDI BILA KUJALI VYAMA VYA SIASA.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Na Hastin Liumba,Igunga
 
UMOJA wa Vijana VCCM  Mkoani Tabora umewataka vijna kuacha kulaumu
viongozi wa seriklai badala yake waunde vikundi vya ujasilia mali ili
serikali iweze kuwapatia mikopo.
 
Mwenyekiti wa  Umoja  huo UVCCM Mkoani Tabora Self  Hamis Gulamali
alisema hayo  katika maadhimisho ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar
yaliyofanyika wilayani Igunga na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa
chama hicho mkoa.
 
Gulamali akiwahutubia wanachama wa chama hicho na wananchi kwa ujumla
alisema vijana wengi hulaumu viongozi wa serikali tu undeni vikundi
bila kujali anatoka CCM au CHADEMA ama vyama vingine.
 
Alisema kuwa endapo vijana wakatumia fulsa zilizopo katika maeneo yao
watanufaika na fulsa hizo ikiwa na kupatiwa mikopo na serikali ambayo
imetenga fungu kubwa kwa kundi hilo la vijana.
 
Alisema  vijana wote mkoani Tabora bila kujali itikadi ya Dini,Kabila
na Siasa wajiunge na vikundi kisha kubuni mradi itakayo weza
kuwasaidia kukopeshwa na Serikali na wao waweze kukopesheka.
 
Mbunge wa Jimbo hilo Dkt,Peter Dalali kafumu aliwataka vijana kuacha
kuwalaum viongozi waliopo madarakani ikiwa na serikali kwa ujumla
badala  yake wabuni miradi ya msingi itakayo wasidia na kuishawishi
serikali itoe mikopo.
 
Mbunge wa Jimbo la sikonge Said Nkumba alisema  serikali iliyopo
madarakani haina ubaguzi kwa vijana wa kada mbalimbali na kuongeza
kuwa kina cho hitajika ni kuunda vikundi.
 
Alisema vijana endepo watajiunga na vikundio wata ongeza pato la Taifa
na kuondoka na umasikini ikiwa na kulaumu vingozi waliopo madarakani
na serikali kwa ujumla.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited : |
Copyright © 2012. Tabora Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za mikoa