Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Ajali mbaya imetokea muda mchache uliopita katika lango Kuu la kuingilia katika Mahakama ya mjini Tabora. Ajali hiyo imehusisha Gari ndogo aina ya Rav 4 yenye usajili wa namba T516 ALA ambayo ilikuwa inaendeshwa na Mama mmoja aliye tambulika kwa jina la Stumai Tambwe ambapo ameigonga Bodaboda iliyokuwa na Abiria na kuwasababishia kuumia vibaya san, na baada ya hapo Gari hilo liligonga mti na kumsababishia kuumia vibaya.
Majeruhi wote wamekimbizwa Hospitali kwa ajili ya Matibabu zaidi na hali zao wote mpaka sasa ni mbaya.
Majeruhi wakipata Msaada baada ya ajali hiyo kutokea mapema leo
Stumai Tambwe Dereva wa Rav 4 aliyesababisha ajali hiyo
Gari baada ya kugonga Bodaboda liligonga Mti na ndipo mama huyo aliumia vibaya.
Dereva wa Boda boda Uromi wakati baada ya kupata ajali, lakini amefariki muda mchache baada ya kufika Hospitali
Hapa ndipo mahali ajali hiyo ilitokea
Picha na Tabora yetu Blog
Picha na Tabora yetu Blog
0 comments:
Post a Comment