Home » » Wachimbaji Nzega kupatiwa eneo

Wachimbaji Nzega kupatiwa eneo

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
MKUU wa Mkoa wa Tabora, Fatuma MwasaMKUU wa Mkoa wa Tabora, Fatuma Mwasa, amesema Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ameridhia eneo namba saba litumiwe na wachimbaji wadogo wa madini.
Amesema taratibu zinaendelea kufanyika na wakati wowote kazi ya uchimbaji itaanza.
Mwasa, alitoa kauli hiyo wilayani hapa juzi kwenye mkutano wa hadhara, wakati wa ziara ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana, inayoendelea mkoani Tabora.
Alisema serikali inawahakikishia wachimbaji wadogo wilayani hapa kuwa wataruhusiwa kuchimba madini eneo hilo.
Akizungumzia mradi wa maji kutoka ziwa Victoria, alisema utakamilika kabla ya mwaka 2015.
Alisema mradi huo ni ahadi ya Rais Jakaya Kikwete aliyoitoa kwa wananchi wa Wilaya ya Nzega na Igunga.
Kwa upande wake, Kinana aliahidi kulipatia ufumbuzi tatizo la wachimbaji wadogo, na kwamba ataendelea kuwasiliana na Waziri Mkuu, ili kujua hatua iliyofikiwa.
 Chanzo:Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited : |
Copyright © 2012. Tabora Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za mikoa