Katibu
Mkuu mstaafu wa Shirikisho la vyama huru vya wafanyakazi (ICFTU/AFRO),
Andrew Kailembo(kulia), akiwa katika mkutano wa wadau mbalimbali wa
kujadili maendeleo ya mkoa wa Kagera uliofanyika jana.
Wakili wa Kujitegemea, wa IMMMA ADVOCATES, Protas Ishengoma akiongoza mkutano huo.
REV.Fr
Kamugisha (kulia), ambaye ni Mkurugenzi wa Hoteli ya Kolping akichangia
mada. Kutoka kushoto ni Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea, Fr, James
Rugemalira na Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali mstaafu, Fabian Masawe.
Wanahabari wa mkoa wa Kagera wakiwa kwenye mkutano huo.
Mkuu
wa Utawala wa Jumuia ya Afrika Mashariki, mstaafu, Abdul Katabaro naye
alipata fursa ya kuchangia katika mkutano huo muhimu wa kuhimiza
uwekezaji mkoani humo.
MSHAURI wa
Kimataifa wa kujitegemea (International Independent Consultant) Fr.
James Rugemalira, wa Mabibo Breweries, jana aliandaa hafla ya
kuzungumzia fursa za maendeleo katika mkoa wa Kagera ndani ya mtangamano
wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Hafla hiyo ilihudhiriwa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali Mstaafu Fabian Massawe, ambaye alikuwa Mgeni Rasmi.
Wengine
waliohudhuria ni pamoja na wana Kagera wanaoishi na kufanya Kazi nje ya
mkoa wa Kagera wakiwemo wakili wa kujitegemea Bw. Protase Ishengoma wa
IMMMA Advocates, mfanyabiashara na Mshauri wa Fr. James, Bw. Abdul
Katabaro ambaye amestaafu kutoka utumishi wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki, Mzee Andrew Kailembo kutoka Bruxelles, Rev. Fr. David na
Kyabukoba, miongoni mwa wengi.
Hafla
hiyo iliyofanyika kwenye hoteli ya Kolping, mjini Bukoba, pia
ilihudhiriwa na waandishi wa habari kutoka kwenye vyombo mbalimbali vya
habari.
Fr.
James alisisitiza juu ya mkoa kuzitumia fursa nyingi za uchumi
zinazotokana na jiografia ya mkoa wa Kagera kupakana na nchi zote za
Jumuiya ya Afrika Mashariki, zikiwemo Burundi, Rwanda, Uganda na Kenya
kwa maana hiyo kuufanya mkoa huo kuwa ndicho kiunganishi cha nchi zote
(hub).
Kwa
sababu hiyo alisisitiza umuhimu wa mkoa wa Kagera kuwa na miradi
mikubwa ya miundombinu ikiwemo ujenzi wa uwanja wa Ki-mataifa
Omukajunguti, ujenzi wa Bandari Kavu na maeneo huru ya Uzalishaji (EPZ)
eneo la Kitengule na kilimo cha Matunda, mboga na mazao mengine ya
chakula. Alisisitiza kuwa soko la mazao lipo katika nchi zinazouzunguka
mkoa wa Kagera.
Fr.
James aliitumia fursa hiyo kuelezea mipango ya kampuni ya Mabibo
Breweries kuwekeza kwenye kiwanda cha kuzalisha bia aina ya Windhoek
katika mikoa ya Kagera, Tanga na Kilimanjaro.
Pia
alizungumzia mpango wa kuanzisha taasisi ya ki mataifa ya uchunguzi na
tiba kwa maradhi ya Kansa kitakachojulikana kama RUTAKWA BYERA
INTERNATIONAL DREAM TANK CANCER CENTER ndani ya Manispaa ya Bukoba.
Naye
Mkuu wa Mkoa alimshukuru sana Fr. James kwa moyo wa uzalendo wa
kuhamasisha uwekezaji katika mkoa wa Kagera na yeye mwenyewe na Mabibo
Breweries kuwa msitari wa mbele kwa vitendo. Kanali Massawe
alimuhakikishia kwamba Serikali ya Mkoa itampatia yeye pamoja na
wawekezaji wengine watakaojitokeza, ushirikiano wa dhati ili kuhakikisha
uchumi wa mkoa unapanuka na kuongeza ajira kwa vijana.
Kanali
Massawe aliwaambia washiriki wa hafla hiyo kuwa alipofika kwenye mkoa
wa Kagera miaka saba iliyopita, mkoa ulikuwa unashika nafasi ya tatu
kutoka mwisho kati ya mikoa 25 katika uchumi lakini sasa mabadiliko
makubwa yamekuwepo mkoa upo kwenye nafasi ya kumi na Sita.
Aliongeza
kusema kwamba kwa fursa zilizopo, endapo zitatumiwa vizuri, basi mkoa
unaweza kufanya vizuri zaidi. Kanali Massawe, aliziainisha fursa nyingi
zilizopo na ambazo hazijasisimiliwa kuwa ni pamoja na Utalii ambao mkoa
unavyo vivutio vingi ikiwa ni pamoja na Ziwa Victoria, mto Kagera, watu
na Utamaduni wao, historia, kituo cha hija cha Nyakijoga na Makanisa
makubwa yaliyojengwa zaidi ya miaka mia moja iliyopita.
Waalikwa
mbalimbali waliopata fursa ya kuongea walimpongeza sana Fr. James kwa
jitihada zake na kuwahamasisha /kuwashirikisha wengine katika kusukuma
gurudumu la maendeleo ya mkoa wa Kagera.
Naye
mwakilishi wa waandishi wa habari waliohudhuria, aliahidi kwamba
watatoa ushirikiano mkubwa wa kuihabarisha jamii kwa ufasaha juu ya
jitihada zote za kusukuma mbele gurudumu la maendeleo
0 comments:
Post a Comment