Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
|
Mgombea
mwenza wa nafasi ya urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mama Samia
Suluhu Hassan akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara wa kampeni
za CCM Kata ya Mabama, Jimbo la Sikonge Tabora. |
|
Mgombea
mwenza wa nafasi ya urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mama Samia
Suluhu Hassan (katikati) akiwapongeza mgombea ubunge wa CCM Jimbo la
Sikonge, George Kakunda na aliyekuwa mpinzani wake katika kura za maoni,
Said Nkumba (kukia) baada ya kumaliza tofauti zao na kuunda timu ya
ushindi wa CCM. |
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
Wagombea nafasi ya udiwani kupitia CCM Sikonge wakiwa katika mkutano wa hadhara jimboni humo. |
|
Mgombea
mwenza wa nafasi ya urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mama Samia
Suluhu Hassan akisalimiana na baadhi ya viongozi na makada wa CCM baada
ya kuwasili Jimbo la Urambo Magharibi alipofanya mkutano wa hadhara. |
|
Aliyekuwa
mgombea ubunge wa Jimbo la Tabora Kaskazini kwa tiketi ya Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Daudi Nteminyanda akizungumza kwenye
mkutano wa kampeni wa CCM leo, ambapo alikiponda chama cha Chadema. |
|
Mgombea
ubunge wa Jimbo la Urambo Magharibi, Magreth Sitta akizungumza na
wananchi katika mkutano wa hadhara wa kampeni za CCM Jimboni humo Mkoa
wa Tabora leo. |
|
Baadhi ya waangalizi wa uchaguzi wenye vizibau wakiwa katika moja ya mikutano ya kampeni za CCM leo. |
|
Kundi
la wasanii wa Bongo Movie makada wa CCM wakiwaburudisha wananchi katika
mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa CCM Jimbo la Urambo Mashariki
Wilaya ya Kaliua leo. |
|
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Sikonge, Said Nkumba akiwa meza kuu katika mkutano wa kampeni wa CCM leo katika Kata ya Maboma. |
|
Mgombea
mwenza wa nafasi ya urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mama Samia
Suluhu Hassan (katikati) akisaini kitabu cha wageni katika mkutano wa
hadhara kampeni za CCM Jimbo la Tabora Kaskazini. Kulia ni Mwenyekiti wa
CCM, Hassan Wakasubi na kushoto ni mgombea ubunge wa Jimbo la Urambo
Mashariki, Juma Kapuya.
[caption id="attachment_62649" align="alignnone" width="300"]
Mgombea ubunge wa Jimbo la Sikonge, George Kakunda akiwahutubia
wananchi katika mkutano wa hadhara wa kampeni za CCM Kata ya Mabama,
Mkoa wa Tabora leo.[/caption]
MGOMBEA mwenza wa nafasi ya urais kwa tiketi ya
Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mama Samia Suluhu Hassan amesema endapo chama
chake kitafanikiwa kushinda na kuunda Serikali kitahakikisha vyama
vyote vya ushirika vya wakulima vinaangaliwa upya ili kuhakikisha
vinawasaidia wakulima.
Alisema wapo baadhi ya viongozi wa vyama vya ushirika
ambao wanavitumia vibaya vyama vya ushirika na kuwanufaisha zaidi wao
zaidi ya wakulima jambo ambalo limekuwa halina manufaa kwao.
"...Tutaviangalia upya vyama vyote vya ushirika ili kuhakikisha tunaweka
viongozi wenye utashi wanaoweza kuwanufaisha wakulima, maana wapo
baadhi ya watu ambao wanajifanya mungu watu...wanataka wao waabudiwe
hili halikubaliki hata kidogo," alisema mgombea mwenza.
Mama Samia Suluhu alisema wamepanga kuiongezea uwezo
taasisi iliyoanzishwa kwa ajili ya kushughulikia kero anuai za walimu
ili iweze kuangalia masuala kama viwango vya mishahara ya walimu,
upandishaji madaraja na vyeo vya walimu pamoja na maslahi mengine ya
wafanyakazi.
Alisema Serikali ya CCM itahakikisha maslahi ya wakulima
na wafanyakazi yanaangaliwa kwa karibu kupitia taasisi maalumu ili
kuchochea ufanisi na uwajibikaji kazini. Alisema ni jambo la kushangaza
kuona wakulima wanalima mazao yao na baadaye kulipwa kwa taabu huku
wakiwa wametumia gharama zao.
Kwa upande wake aliyekuwa mgombea ubunge wa Jimbo la
Tabora Kaskazini kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA), Daudi Nteminyanda aliwaomba wananchi kukinyima kura chama
hicho kwani hakina viongozi waadilifu zaidi ya viongozi maslahi. Alisema
viongozi wa CHADEMA ni vigeugeu ambao hawapaswi kupewa uongozi wa nchi
kwa kile kuwakumbatia watu kiliokuwa kikuwaita mafisadi hapo awali
lakini leo kimewapa nyazifa za juu.
Kiongozi huyo wa Chadema ambaye alishinda kura za maoini
katika nafasi yake na baadaye kukatwa nafasi yake kisha kupewa aliyekuwa
kada wa CCM, Josef Kidaha aliyehamia Chadema kwa sasa amekikimbia chama
cha Chadema na kujiunga na CCM, huku akikinadi ndiyo chama pekee
shupavu kitakachoreta maendeleo.
Mama Samia Suluhu leo amemaliza ziara ya kampeni Mkoani
Tabora baada ya kufanya mikutano ya kampeni katika majimbo ya Urambo
Magharibi, Urambo Mashariki, Tabora Kaskazini-Uyui, na Jimbo la Sikonge.
Kesho anaelekea Mkoa wa Kigoma kuendelea na ziara yake ya kampeni
kunadi ilani ya CCM.
*Imeandaliwa na www.thehabari.com |
0 comments:
Post a Comment