Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Diwani
wa kata ya Mitundu, tarafa ya Itigi,wilayani Manyoni, Bwana Andrea
Madole (kushoto) akiteta jambo na Mwenyekiti wa Kijiji cha Mitundu
wakati akijiandaa kuongea na wananchi wa kata hiyo.
Diwani
wa kata ya Mitundu, Bwana Andrea Madole akiongea na wananchi wa kata ya
Mitundu kuwashukuru kwa kumchagua sambamba na kujadiliana sababu za
kata ya Mitundu kutokuwa makao makuu ya Halmashauri ya wilaya ya Itigi.
Afisa mtendaji wa kata ya Mitundu, Bwana Kidolezi (wa kwanza kutoka
kulia) akiandaa kutoa maagizo ya serikali muda mfupi kabla ya kumalizika
kwa mkutano huo wa diwani.
Baadhi
ya wakazi wa kata ya Mitundu waliohudhuria kwenye mkutano uliotishwa na
diwani wa kata hiyo kujadili masuala muhimu ya kimaendeleo.(Picha zote
na Jumbe Ismailly).
Na Jumbe Ismailly, Itigi
ZAIDI
ya wakazi 23,000 wa kata ya Mitundu, tarafa ya Itigi, wilayani Manyoni,
Mkoani Singida wametishia kuihama Halmashauri hiyo na kuhamia
Halmashauri ya wilaya ya Sikonge, Mkoani Tabora endapo makao makuu ya
Halmashauri hiyo hayatakuwa kwenye kata ya Mitundu.
Wakazi
hao wametoa tamko hilo kwenye mkutano wa hadhara ulioitishwa na diwani
wa kata hiyo,Andrea Madole Mkwava kwa lengo la kuwashukuru wananchi kwa
kumchagua pamoja na kujadiliana sababu za kata ya Itigi kuwa makao makuu
ya Halmashauri badala ya kata ya Mitundu kutokuwa makao makuu ya
Halmashauri hiyo.
Aidha
katika mkutano huo uliokuwa chini ya mwenyekiti wa kamati ya maendeleo
ya kata hiyo,wakazi hao walifafanua kwamba hawaoni maana yeyote ya
kudanganywa katikati ya Halmashauri hiyo ni Mji mdogo wa Itigi,wakati
wananchi wa kata za Rungwa,Mwamagembe na Kintanula watakuwa bado
wanafuata huduma za kijamii umbali mrefu.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti mkutanoni hapo,wakazi hao,Sidney David Polepole
alibainisha kuwa serikali iliona umuhimu wa kuigawa wilaya ya Manyoni
kutokana na ukubwa wake iliokuwepo,lakini cha kushangaza watendaji wa
wilaya ya Manyoni wametoa upendeleo kwa mji wa Itigi badala ya kufuata
ukweli kuwa Mitundu ndiyo ingestahili kuwa makao makuu ya Halmashauri ya
Itigi.
Naye
Shabani Makala alisema hakuna sababu za kupiga kura za kuamua ni wapi
sehemu inayostahili kuwa makao makuu ya Halmashauri ya wilaya ya
Itigi,kwani kwa ufahamu wake mdogo anaelewa kwamba agizo likitoka ngazi
za juu huwa linatekelezwa tu,na kuhoji kwamba je huyo mkurugenzi
anapingana na agizo la aliyekuwa waziri mkuu,Mizengo Pinda ambaye naye
anatambua kuwa Mitundu ndiyo katikati ya kata zote za Halmashauri hiyo.
Kwa
upande wake Habibu Ismaili aliweka wazi pia kuwa tangu mwaka 1977
wakazi wa kata hiyo wamekuwa wakiishi maisha ya ukiwa na ndicho chanzo
cha manyanyaso yote wanayofanyiwa maana tangu kipindi hicho
walipotembelewa na rais wa nchi mpaka leo hakuna aliyewahi kuwenda huko.
“Kutokwenda
kwa Raisi kwenye maeneo hayo ya pembezoni kunakosababishwa na watendaji
wa wilaya ya Manyoni kunalazimisha viongozi wakuu kutofahamu kero zao
zinazowakabili na haitakuwa rahisi hata kutambua iwapo maeneo hayo kuna
binadamu au wanyama peke yao ndiyo wanaoishi.”alisisitiza huku
akishangiliwa na wananchi.
Graidesi
Ikunya ni mkazi wa Kijiji cha Mitundu anasisitiza kuwa makao makuu ya
halmashauri ya itigi haiwezekani kabisa kuwa Itigi,lakini kutokana na
ukiritimba uliokuwepo siku za nyuma ndiyo ambao ulisababisha makao makuu
kuwekwa Itigi.
Akizungumza
katika mkutano wa kuwashukuru wananchi sambamba na kuhoji uhalali wa
Itigi kuwa makao makuu ya Halmashauri ya wilaya hiyo,diwani wa kata ya
Mitundu,Andrea Madole Mkwava alisema kwa mujibu wa maelezo ya diwani
aliyemaliza muda wake ni kwamba kutokana na ukubwa wa wilaya hiyo
walipendekeza waombe wilaya na makao makuu yawe Mitundu,lakini baada ya
kupatikana maamuzi yao yamebadilishwa.
0 comments:
Post a Comment