Naibu Waziri Ofisiya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina kulia akifafanua jambo kuhusu utunzaji wa mazingira alipokuwa akiongea na uongozi wa Mkoa wa Tabora (hawapo pichani) leo katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe Aggrey Mwamri na kushoto ni Katibu tawala wa Mkoa Dk. Thea M. Mtara.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora Dk. Thea Mtara akisoma Repoti
ya Mazingira ya Mkoa kwa Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na
Mazingira Mhe Luhaga Mpina mapema leo kabla ya kuanza ziara ya ukaguzi wa
mazingira Mkoani Tabora.
Pichani sehemu ya washiriki wa mkutano wa viongozi wa Mkoa wa
Tabora na waandishi wa habari wakati Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais
Muungano namazingira Mhe. Luhaga Mpina akipokea maelezo kuhusu ripoti ya
mazingira ya Mkoa wa Tabora. (Habari na Picha na Evelyn Mkokoi.)
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira
Mhe Luhaga Mpina, amewataka viongozi wa Mkoa wa Tabora kuwachukulia hatua za
kisheria waharibifu wa mazingira mkoani humo, na kushauri Mahakama kuongeza jitihada kwa
kuhakikisha mazingira yanalindwa kwa kusikiliza haraka kesi za uharibifu wa mazingira
zinazopelekwa mahakamani na pia ziende kwa wakati.
Mpina ameyasema hayo Mkoani Tabora alipokuwa akipokea repoti
ya mazingira ya Mkoa iliyosomwa na
katibu tawala wa mkoa Dkt Thea Mtara mapema leo kabla ya kuanza ziara yake ya
ukaguzi wa mazingira mkoani humo.
Aliongeza kuwa suala la usafi wa mazingira linapaswa kupewa
kipaumbele na ifikie mahali kila Halmashauri na manisapaa itoe ripoti yaukweli
kuhusu usafi wa mazingira na upandani wa miti katika halmashauri zao na
watendaji wavivu na wasiojiweza wafukuzwe kazi na kuchukuliwa hatua.
Naibu Waziri Mpina aliongeza kwa kusema kuwa hakuna haja ya
kuwa na vyombo vya utendaji kama NEMC au wakala wa taifa wa misitu katika kila
kijiji kwani mfumo wa selikali uliyo
unajitosheleza, hivyo kila mtumishi anapaswa kuwajibika kwanafasi yake.
“nimeskia kumekuwa na uharibifu wa mazingira hapa Tabora
unaofanywa na wachimbaji wadogo pia na wawekezaji, tuna haja ya kujirithisha
kama wawekezaji hawa wanafuata sheria za nchi kama vile kupata vyeti vya mazingira kupitia Baraza la Hiafadhi na
Usmamizi wa Mazingira (NEMC).” Alisisitiza Mpina.
Awali, akisoma Ripoti ya mazingira ya Mkoa wa Tabora, katibu
Tawala wa Mkoa huo Dk. Thea Mtara, alisema kuwa mkoa umekuwa uikabiliwa na
changamoto mbali mbali za uharibifu wa mazingira ikiwa ni pamoja na uchimbaji wa kokoto, uharibifu wa
kukoboa miti kwa ajili yahifadhi ya tumbaku, uchimbaji wa madini na uharibifu katika
hifadhi za taifa kutokana na uvamizi wakulima na wafugaji.
Lengo la ziara ya Naibu Waziri Mpina Mkoani Tabora
inahusisha ukaguzi wa mazingira, ukaguzi
wa utekelezaji wa agizo la serikali la kupanda miti na ufuatiliaji wa swala
zima la usafi wa mazingira mkoani Tabora ambapo Ripoti ya Mkoa inaema kwa
upande wa swala la usafi wa Mazingira Mkoa umejitahidi.
0 comments:
Post a Comment